Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Yoshua 10:29, 30
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 29 Kisha Yoshua na Waisraeli wote wakatoka Makeda na kwenda Libna, wakalishambulia jiji la Libna.+ 30 Yehova akalitia pia jiji hilo na mfalme wake+ mikononi mwa Waisraeli, wakalishambulia na kuwaangamiza wakaaji wote kwa upanga, na hakuna yeyote aliyebaki humo. Wakamtendea mfalme wake kama walivyomtendea mfalme wa Yeriko.+

  • 2 Wafalme 8:22
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 22 Lakini tangu siku hiyo Waedomu wameendelea kuiasi nchi ya Yuda. Watu wa Libna+ waliasi pia wakati huo.

  • 2 Wafalme 19:8-13
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 8 Baada ya Rabshake kusikia kwamba mfalme wa Ashuru ameondoka Lakishi,+ alirudi na kumkuta akipigana vita na Libna.+ 9 Ndipo mfalme akasikia maneno haya yakisemwa kumhusu Tirhaka mfalme wa Ethiopia: “Ametoka ili kuja kupigana nawe.” Kwa hiyo akawatuma tena wajumbe+ kwa Hezekia, akisema: 10 “Mwambieni hivi Mfalme Hezekia wa Yuda: ‘Usikubali Mungu wako unayemtumaini akudanganye akisema: “Yerusalemu halitatiwa mikononi mwa mfalme wa Ashuru.”+ 11 Tazama! Umesikia mambo ambayo wafalme wa Ashuru walizitendea nchi zote kwa kuziangamiza.+ Je, ni wewe peke yako utakayeokolewa? 12 Je, miungu ya mataifa yaliyoangamizwa na mababu zangu iliyaokoa mataifa hayo? Gozani, Harani,+ Resefu, na watu wa Edeni waliokuwa Tel-asari wako wapi? 13 Yuko wapi mfalme wa Hamathi, mfalme wa Arpadi, na mfalme wa majiji ya Sefarvaimu, na wa Hena, na wa Iva?’”+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki