-
2 Wafalme 17:5, 6Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Mfalme wa Ashuru aliivamia nchi nzima, naye akaja Samaria na kulizingira kwa miaka mitatu. 6 Katika mwaka wa tisa wa utawala wa Hoshea, mfalme wa Ashuru aliliteka jiji la Samaria.+ Kisha akawapeleka Waisraeli uhamishoni+ kule Ashuru na kuwaweka katika eneo la Hala na Habori kando ya mto Gozani+ na katika majiji ya Wamedi ili waishi humo.+
-