17 Mtu mmoja katika umati akamjibu: “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako kwa sababu ana roho anayemfanya awe bubu.+ 18 Kila mara anapomshambulia humwangusha chini, naye hutoa povu mdomoni na kusaga meno yake na kuishiwa nguvu. Niliwaambia wanafunzi wako wamfukuze, lakini hawakuweza.”