Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 17:14-17
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 14 Walipofika karibu na umati,+ mtu fulani akamkaribia Yesu, akapiga magoti, na kusema: 15 “Bwana, mhurumie* mwanangu, kwa sababu ana kifafa na ni mgonjwa sana. Yeye huanguka ndani ya moto na ndani ya maji mara nyingi.+ 16 Nilimleta kwa wanafunzi wako, lakini walishindwa kumponya.” 17 Yesu akajibu: “Enyi kizazi kisicho na imani na kilichopotoka,+ nitaendelea kuwa pamoja nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni hapa.”

  • Luka 9:38-42
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 38 Na tazama! mtu fulani katika umati akasema kwa sauti kubwa: “Mwalimu, ninakuomba umwangalie mwanangu, kwa sababu yeye ni mwanangu wa pekee.+ 39 Tazama! roho mwovu humshika, naye hupiga kelele ghafla, na humfanya agaegae na kutokwa na povu mdomoni, naye hamtoki upesi mpaka anapomjeruhi. 40 Niliwaomba wanafunzi wako wamfukuze, lakini wakashindwa.” 41 Yesu akajibu: “Enyi kizazi kisicho na imani na kilichopotoka,+ nitaendelea kuwa pamoja nanyi na kuwavumilia mpaka lini? Mlete mwanao hapa.”+ 42 Lakini alipokuwa akikaribia, yule roho mwovu akamwangusha na kumfanya agaegae sana. Hata hivyo, Yesu akamkemea yule roho mwovu na kumponya mvulana huyo, kisha akamkabidhi kwa baba yake.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki