-
Yoshua 21:20-26Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
20 Na Walawi waliobaki wa koo za Wakohathi walipewa majiji kwa kura katika eneo la kabila la Efraimu. 21 Waliwapa jiji la makimbilio kwa ajili ya muuaji,+ yaani, jiji la Shekemu+ na malisho yake katika eneo lenye milima la Efraimu, Gezeri+ na malisho yake, 22 Kibsaimu na malisho yake, na Beth-horoni+ na malisho yake—majiji manne.
23 Na katika eneo la kabila la Dani: Elteke na malisho yake, Gibethoni na malisho yake, 24 Aiyaloni+ na malisho yake, Gath-rimoni na malisho yake—majiji manne.
25 Na katika eneo la nusu ya kabila la Manase: Taanaki+ na malisho yake na Gath-rimoni na malisho yake—majiji mawili.
26 Koo zilizobaki za Wakohathi zilipewa jumla ya majiji kumi na malisho yake.
-