27 Hiramu akawatuma watumishi wake mwenyewe, mabaharia wenye uzoefu, wakafanye kazi pamoja na watumishi wa Sulemani kwenye kundi hilo la meli.+28 Wakaenda Ofiri,+ wakachukua talanta 420 za dhahabu na kumletea Mfalme Sulemani.
22 Mfalme alikuwa na kundi la meli za Tarshishi+ baharini pamoja na kundi la meli za Hiramu. Mara moja baada ya kila miaka mitatu, kundi la meli za Tarshishi zilikuja zikiwa zimejazwa dhahabu na fedha, pembe za tembo,+ sokwe, na tausi.
18 Hiramu+ aliwatuma watumishi wake mwenyewe wampelekee meli na mabaharia wenye uzoefu. Wakaenda Ofiri+ pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua huko talanta 450* za dhahabu+ na kumletea Mfalme Sulemani.+