Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 2 Wafalme 10:10-14
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 10 Basi jueni kwamba hakuna neno hata moja la Yehova ambalo Yehova amesema dhidi ya nyumba ya Ahabu litakalokosa kutimia,*+ na Yehova amefanya yale aliyosema kupitia mtumishi wake Eliya.”+ 11 Basi Yehu akawaua watu wote waliobaki wa nyumba ya Ahabu kule Yezreeli, na pia watu wake wote mashuhuri, marafiki zake, na makuhani wake,+ hakumwacha mtu yeyote wa nyumba yake akiwa hai.+

      12 Kisha akaondoka na kuelekea Samaria. Njiani kulikuwa na nyumba ya kuwakatia kondoo manyoya. 13 Huko Yehu akakutana na ndugu za Mfalme Ahazia+ wa Yuda, naye akawauliza, “Ninyi ni nani?” Wakasema: “Sisi ni ndugu za Ahazia, nasi tunashuka kwenda kuwajulia hali wana wa mfalme na wana wa mama malkia.” 14 Mara moja akasema: “Wakamateni wakiwa hai!” Basi wakawakamata wanaume 42 wakiwa hai na kuwachinja kando ya tangi la maji la nyumba ya kuwakatia kondoo manyoya. Hakumwacha yeyote kati yao akiwa hai.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki