-
2 Wafalme 11:5-8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
5 Akawapa agizo hili: “Hivi ndivyo mtakavyofanya: Theluthi moja watashika zamu siku ya Sabato, na kuweka ulinzi mkali katika nyumba ya* mfalme,+ 6 theluthi nyingine watakuwa katika Lango la Msingi, na theluthi nyingine watakuwa katika lango lililo nyuma ya walinzi wa jumba la mfalme. Mtalinda nyumba hiyo kwa zamu. 7 Vikundi vyenu viwili ambavyo havipaswi kuwa na zamu siku ya Sabato vinapaswa kuweka ulinzi mkali katika nyumba ya Yehova ili kumlinda mfalme. 8 Mnapaswa kumzunguka mfalme pande zote, kila mmoja akiwa na silaha zake mikononi mwake. Yeyote atakayekaribia kikosi hicho atauawa. Mfuateni mfalme popote aendapo.”*
-
-
1 Mambo ya Nyakati 9:22-25Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
22 Wote waliochaguliwa kuwa walinzi kwenye vizingiti walikuwa 212. Waliishi katika vijiji vyao kulingana na orodha ya ukoo wao.+ Daudi na Samweli yule mwonaji+ waliwaweka katika wadhifa wa kuaminiwa. 23 Watu hao pamoja na wana wao walisimamia utumishi wa ulinzi wa malango ya nyumba ya Yehova,+ nyumba ya hema. 24 Walinzi wa malango walikuwa pande zote nne—mashariki, magharibi, kaskazini, na kusini.+ 25 Mara kwa mara, ndugu zao walipaswa kuja kwa siku saba kutoka katika vijiji vyao ili kutumikia pamoja nao.
-