Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • 1 Wafalme 6:23-28
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 23 Katika chumba cha ndani zaidi alitengeneza makerubi wawili+ kwa mbao za msonobari,* kila kerubi alikuwa na kimo cha mikono kumi.+ 24 Bawa moja la kerubi lilikuwa na urefu wa mikono mitano, na bawa lingine lilikuwa na urefu wa mikono mitano. Urefu kutoka ncha ya bawa moja mpaka ncha ya bawa lingine ulikuwa mikono kumi. 25 Kerubi wa pili alikuwa pia na kimo cha mikono kumi. Makerubi wote wawili walikuwa na ukubwa uleule na umbo lilelile. 26 Kimo cha kerubi mmoja kilikuwa mikono kumi, sawa na kimo cha kerubi wa pili. 27 Kisha akawaweka makerubi+ hao ndani ya chumba cha ndani zaidi cha nyumba hiyo.* Mabawa ya makerubi hao yalikunjuliwa hivi kwamba bawa la kerubi moja lilifika kwenye ukuta mmoja na bawa la kerubi mwingine lilifika kwenye ukuta wa pili, na mabawa yao yalipanuka kuelekea katikati ya nyumba hiyo, hivi kwamba yaligusana. 28 Naye aliwafunika makerubi hao kwa dhahabu.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki