-
2 Mambo ya Nyakati 3:10-13Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
10 Kisha akatengeneza mifano ya makerubi wawili katika chumba cha Patakatifu Zaidi,* akawafunika kwa dhahabu.+ 11 Kwa ujumla mabawa ya makerubi hao+ yalikuwa na urefu wa mikono 20; bawa moja la kerubi wa kwanza lilikuwa na urefu wa mikono mitano nalo liligusa ukuta wa nyumba, na bawa la pili lilikuwa na urefu wa mikono mitano nalo liligusa bawa moja la kerubi wa pili. 12 Na bawa moja la kerubi wa pili lilikuwa na urefu wa mikono mitano nalo liligusa ukuta wa nyumba, na bawa la pili lilikuwa na urefu wa mikono mitano nalo liligusa bawa moja la yule kerubi wa kwanza. 13 Mabawa ya makerubi hao yalikuwa yamenyooshwa kufikia urefu wa mikono 20; nao walikuwa wamesimama kwa miguu yao, nyuso zao zikielekea ndani.*
-