26 Mfalme Sulemani akatengeneza pia kundi la meli katika jiji la Esion-geberi,+ lililo kando ya Elothi, ufuoni mwa Bahari Nyekundu katika nchi ya Edomu.+
6 Wakati huo Mfalme Resini wa Siria akarudisha Elathi+ kwa Edomu, kisha akawafukuza Wayahudi* kutoka Elathi. Na Waedomu wakaingia Elathi, nao wamekuwa wakiishi humo tangu wakati huo.