29 “Yehova Mungu wenu atakapoyaangamiza mataifa ambayo mtamiliki nchi yao,+ na mtakapokuwa mkiishi katika nchi yao, 30 jihadharini msinaswe baada ya mataifa hayo kuangamizwa kutoka mbele yenu. Msiulize hivi kuhusu miungu yao: ‘Mataifa haya yaliabuduje miungu yake? Mimi pia nitafanya vivyo hivyo.’+