-
Kumbukumbu la Torati 15:1-3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
15 “Mwishoni mwa kila miaka saba mnapaswa kufuta madeni.+ 2 Hivi ndivyo mtakavyoyafuta: Kila mtu aliyemkopesha jirani yake atafuta deni hilo. Hapaswi kudai malipo kutoka kwa jirani au ndugu yake, kwa maana yatatangazwa yamefutwa kwa agizo la Yehova.+ 3 Mnaweza kudai malipo kutoka kwa mgeni,+ lakini mnapaswa kufuta deni lolote la ndugu yenu.
-