-
Matendo 12:21-23Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
21 Siku moja iliyochaguliwa, Herode alivaa mavazi ya kifalme akaketi kwenye kiti cha hukumu na kuanza kuwahutubia watu wote. 22 Ndipo watu waliokusanyika wakaanza kusema kwa sauti kubwa: “Hii ni sauti ya mungu, si ya mwanadamu!” 23 Papo hapo, malaika wa Yehova* akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu, naye akaliwa na wadudu akafa.
-