23 Ahithofeli alipoona kwamba ushauri wake haukufuatwa, aliweka matandiko juu ya punda wake na kwenda nyumbani kwake katika mji wao.+ Baada ya kuwapa maagizo watu wa nyumbani mwake,+ akajitia kitanzi.*+ Basi akafa na kuzikwa katika makaburi ya mababu zake.
14 Ndipo Yoabu akasema: “Sitaendelea kupoteza muda pamoja nawe!” Basi akachukua mikuki mitatu midogo* na kumchoma nayo Absalomu kwenye moyo alipokuwa angali hai akining’inia kwenye mti mkubwa.