2 Kwa hiyo Yehova akawatia mikononi mwa* Yabini mfalme wa Kanaani,+ aliyetawala Hasori. Mkuu wa jeshi lake aliitwa Sisera, naye aliishi Haroshethi+ ya mataifa.*
15 Kisha Yehova akamvuruga+ Sisera na magari yake yote ya vita na jeshi lake lote na kuwaangamiza kwa upanga wa Baraka. Ndipo Sisera akatoka katika gari lake na kukimbia kwa miguu.