-
Kutoka 10:13-15Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
13 Mara moja Musa akainyoosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na Yehova akasababisha upepo wa mashariki uvume nchini mchana kutwa na usiku kucha. Asubuhi ilipofika, upepo huo wa mashariki ukaleta nzige. 14 Na nzige hao wakaja juu ya nchi yote ya Misri na kufunika eneo lote la Misri.+ Walikuwa wengi kupindukia;+ nzige wengi sana hivyo hawakuwa wamewahi kuonekana, wala nzige wengi sana hivyo hawangeonekana tena kamwe. 15 Waliifunika nchi yote, na nchi ikawa na giza kwa sababu yao; walitafuna mimea yote nchini na matunda yote mitini ambayo hayakuharibiwa na mvua ya mawe; hakuna majani yoyote yaliyobaki mitini wala kwenye mimea ya shambani katika nchi yote ya Misri.
-