Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mwanzo 33:4, 5
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 4 Lakini Esau akakimbia kukutana naye, akamkumbatia na kumbusu, nao wakatokwa na machozi. 5 Alipoinua macho yake na kuona wanawake na watoto, akauliza: “Ni nani hawa walio pamoja nawe?” Yakobo akamwambia: “Ni watoto ambao Mungu amenipa kwa fadhili mimi mtumishi wako.”+

  • Mwanzo 48:3, 4
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 3 Yakobo akamwambia Yosefu:

      “Mungu Mweza-Yote alinitokea kule Luzi katika nchi ya Kanaani na kunibariki.+ 4 Naye akaniambia, ‘Ninakufanya uzae, nami nitakufanya uwe na watoto wengi, nami nitakufanya uwe kusanyiko la mataifa,+ nami nitaupa uzao wako* baada yako nchi hii iwe miliki yao ya kudumu.’+

  • 1 Samweli 2:21
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 21 Yehova akamkazia uangalifu Hana, ili aweze kupata mimba;+ basi akazaa wana watatu zaidi na mabinti wawili. Naye mvulana Samweli akaendelea kukua mbele za Yehova.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki