-
Mwanzo 37:9-11Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 Baada ya hayo akaota tena ndoto nyingine, naye akawasimulia ndugu zake ndoto hiyo: “Nimeota ndoto nyingine. Wakati huu jua na mwezi na nyota 11 zilikuwa zikiniinamia.”+ 10 Kisha akamsimulia baba yake na ndugu zake ndoto hiyo, baba yake akamkemea na kumuuliza: “Ndoto hiyo yako inamaanisha nini? Je, kweli mimi na pia mama yako na ndugu zako tutakuja na kukuinamia mpaka ardhini?” 11 Basi ndugu zake wakazidi kumwonea wivu,+ lakini baba yake akayaweka akilini maneno yake.
-