-
Kumbukumbu la Torati 28:63, 64Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
63 “Na kama Yehova alivyopendezwa wakati mmoja kuwafanikisha na kuwafanya mwongezeke, ndivyo Yehova atakavyopendezwa kuwaharibu na kuwaangamiza; nanyi mtang’olewa kutoka katika nchi mnayokaribia kuimiliki.
64 “Yehova atawatawanya miongoni mwa mataifa yote, kutoka mwisho mmoja wa dunia mpaka mwisho mwingine wa dunia,+ na huko mtalazimika kuabudu miungu ya miti na mawe, ambayo wala ninyi wala mababu zenu hamwijui.+
-