17 Kama vile mwanamke mwenye mimba aliye karibu kuzaa
Anavyopata maumivu na kulia kwa uchungu,
Ndivyo hali yetu ilivyo kwa sababu yako, Ee Yehova.
18 Tulipata mimba, tulikuwa na maumivu ya kuzaa,
Lakini ni kama tumezaa upepo.
Hatujaleta wokovu nchini,
Na hakuna mtu aliyezaliwa ili aishi nchini.