-
Yeremia 44:12Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
12 Nami nitawachukua watu wa Yuda waliobaki walioazimia kwenda nchini Misri kukaa huko, na wote wataangamia nchini Misri.+ Watauawa kwa upanga na kuangamia kwa njaa kali; kuanzia mdogo zaidi mpaka mkubwa zaidi, watakufa kwa upanga na kwa njaa kali. Nao watakuwa laana, kitu cha kutisha, matusi, na shutuma.+
-
-
Ezekieli 17:17, 18Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
17 Na lile jeshi kubwa na wanajeshi wengi wa Farao hawatamsaidia kamwe vitani,+ wakati boma la kuzingira litakapojengwa na kuta za kuzingira zitakapojengwa ili kuangamiza uhai wa* watu wengi. 18 Amedharau kiapo na kuvunja agano. Hata ingawa alitoa ahadi,* amefanya mambo hayo yote, naye hataponyoka.”’
-