-
Ezekieli 1:19-21Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
19 Wakati wowote viumbe hai waliposonga, yale magurudumu yalisonga pamoja nao, na wale viumbe hai walipoinuliwa kutoka duniani, yale magurudumu yaliinuliwa juu pia.+ 20 Walienda popote ambapo roho iliwaelekeza kwenda, popote roho ilipoenda. Magurudumu yaliinuliwa pamoja nao, kwa maana roho iliyokuwa ikitenda katika wale viumbe hai* ilikuwa pia katika yale magurudumu. 21 Waliposonga, magurudumu hayo yalisonga; na waliposimama tuli, nayo yalisimama tuli; na walipoinuliwa juu kutoka duniani, magurudumu yaliinuliwa juu pamoja nao, kwa maana roho iliyokuwa ikitenda katika wale viumbe hai ilikuwa pia katika yale magurudumu.
-