-
Yeremia 25:9Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
9 ninaziita familia zote za kaskazini,”+ asema Yehova, “ninamwita Mfalme Nebukadneza* wa Babiloni, mtumishi wangu,+ nami nitawaleta dhidi ya nchi hii+ na dhidi ya wakaaji wake na dhidi ya mataifa haya yote yanayozunguka.+ Nitawaangamiza na kuwafanya kuwa kitu cha kutisha na kitu cha kupigiwa mluzi na magofu ya kudumu.
-
-
Danieli 3:4, 5Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
4 Mpiga mbiu akatangaza hivi kwa sauti kubwa: “Enyi watu wa makabila, mataifa, na lugha zote, mnaamriwa kwamba, 5 wakati mtakaposikia sauti ya pembe, zumari, zeze, kinubi cha pembe tatu, kinanda, zumari-tete, na ala nyingine zote za muziki, lazima mwanguke chini na kuabudu sanamu ya dhahabu ambayo Mfalme Nebukadneza amesimamisha.
-