48 Kisha mfalme akampandisha cheo Danieli na kumpa zawadi nyingi bora, naye akamfanya kuwa mtawala wa mkoa wote wa* Babiloni+ na msimamizi mkuu wa wanaume wote wenye hekima wa Babiloni.
13 Kwa hiyo Danieli akaletwa mbele ya mfalme. Mfalme akamuuliza Danieli: “Je, wewe ndiye Danieli, mmojawapo wa watu waliohamishwa na baba yangu mfalme kutoka Yuda?+
29 Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvisha Danieli mavazi ya zambarau na mkufu wa dhahabu shingoni mwake; wakatangaza kwamba atakuwa mtawala wa tatu katika ufalme.+