-
2 Wafalme 3:26, 27Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
26 Mfalme wa Moabu alipoona kwamba ameshindwa vitani, akachukua wanaume 700 waliojihami kwa mapanga ili wapenye na kuingia kwa mfalme wa Edomu;+ lakini hawakuweza. 27 Basi akamchukua mwana wake mzaliwa wa kwanza ambaye angetawala baada yake akamtoa kuwa dhabihu ya kuteketezwa+ juu ya ukuta. Wamoabu wakawa na ghadhabu kali dhidi ya Waisraeli, kwa hiyo Waisraeli wakaacha kumshambulia mfalme huyo na kurudi katika nchi yao.
-