-
Malaki 3:2, 3Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
2 “Lakini ni nani atakayestahimili siku atakayokuja, na ni nani atakayeweza kusimama atakapotokea? Kwa maana atakuwa kama moto wa msafishaji wa madini na kama sabuni+ ya wafuaji wa nguo. 3 Naye ataketi kama msafishaji na mtakasaji wa fedha,+ naye atawatakasa wana wa Lawi; atawasafisha kama dhahabu na kama fedha, nao hakika watakuwa watu wanaomtolea Yehova zawadi kwa uadilifu.
-