-
Kumbukumbu la Torati 14:8Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
8 Pia, msimle nguruwe kwa sababu ana kwato zilizopasuka lakini hacheui. Yeye si safi kwenu. Msile kamwe nyama yao wala kugusa mizoga yao.
-
-
Luka 8:31-34Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
-
-
31 Nao wakaendelea kumsihi asiwaamuru waende katika shimo refu lisilo na mwisho.*+ 32 Sasa kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe+ waliokuwa wakila mlimani, basi wakamsihi awaruhusu waingie ndani ya nguruwe hao, naye akawaruhusu.+ 33 Ndipo wale roho waovu wakamtoka mtu huyo na kuingia ndani ya wale nguruwe, kisha lile kundi likatimua mbio, likaruka poromoko,* likazama ndani ya ziwa na kufa maji. 34 Wachungaji walipoona kilichotokea, wakakimbia na kupeleka habari hizo jijini na mashambani.
-