Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 6:21-29
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 21 Nafasi ilipatikana Herode alipoandaa mlo wa jioni kwenye sherehe ya sikukuu yake ya kuzaliwa.+ Akawaalika maofisa wake wa cheo cha juu, makamanda wa jeshi, na watu mashuhuri zaidi wa Galilaya.+ 22 Binti ya Herodia akaingia, akacheza dansi na kumfurahisha Herode na wageni wake.* Mfalme akamwambia msichana huyo: “Niombe chochote unachotaka, nami nitakupa.” 23 Ndiyo, akamwapia: “Chochote utakachoomba nitakupa, hata ikiwa ni nusu ya ufalme wangu.” 24 Akaondoka na kwenda kumuuliza mama yake: “Niombe nini?” Akamwambia: “Kichwa cha Yohana Mbatizaji.” 25 Akarudi haraka mbele ya mfalme na kutoa ombi lake, akisema: “Nataka unipe sasa hivi kwenye sinia kichwa cha Yohana Mbatizaji.”+ 26 Ingawa mfalme alihuzunika sana, hakutaka kupuuza ombi lake, kwa sababu ya viapo vyake na wageni wake.* 27 Mara moja mfalme akamtuma mlinzi na kumwamuru alete kichwa cha Yohana. Basi akaenda gerezani na kumkata kichwa, 28 akakileta kwenye sahani. Akampa yule msichana, na huyo msichana akampa mama yake. 29 Wanafunzi wake waliposikia jambo hilo, wakaja na kuuchukua mwili wake wakaulaza kaburini.*

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki