Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 6:45-52
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 45 Kisha, bila kukawia, akawaagiza wanafunzi wake wapande mashua watangulie kuelekea Bethsaida ng’ambo ya bahari, huku yeye akiuaga umati.+ 46 Lakini baada ya kuwaaga, akaenda mlimani kusali.+ 47 Ilipofika jioni, mashua ilikuwa katikati ya bahari, lakini yeye alikuwa peke yake kwenye nchi kavu.+ 48 Alipowaona wanafunzi wake wakitaabika kupiga makasia kwa kuwa upepo ulikuwa ukivuma kinyume chao, usiku karibu kesha la nne* akawaendea akitembea juu ya bahari; lakini alitaka* kuwapita. 49 Walipomwona akitembea juu ya bahari wakafikiri: “Ni mzuka!” Nao wakapaza sauti. 50 Kwa maana wote walimwona, wakahangaika. Lakini mara moja akawaambia: “Jipeni moyo! Ni mimi; msiogope.”+ 51 Kisha akapanda kwenye mashua, na upepo ukatulia. Nao wakashangaa sana, 52 kwa maana hawakuwa wamefahamu maana ya ule muujiza wa mikate, bado mioyo yao ilikuwa mizito isiweze kuelewa.

  • Yohana 6:16-21
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 16 Ilipofika jioni, wanafunzi wake wakashuka kwenda baharini,+ 17 wakapanda mashua ili wavuke bahari kwenda Kapernaumu. Sasa giza lilikuwa limeingia na bado Yesu hakuwa pamoja nao.+ 18 Pia, bahari ikaanza kuchafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa ukivuma.+ 19 Hata hivyo, walipokuwa wamepiga makasia umbali wa karibu kilomita tano au sita,* wakamwona Yesu akitembea juu ya bahari akiikaribia mashua, nao wakaogopa. 20 Lakini akawaambia: “Ni mimi; msiogope!”+ 21 Basi walitaka kumbeba Yesu kwenye mashua, na mara moja mashua ikafika kwenye nchi kavu mahali walipokuwa wakienda.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki