17 Kwa maana alipokea kutoka kwa Mungu Baba heshima na utukufu alipoambiwa maneno kama haya* kwa utukufu wenye fahari: “Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ambaye mimi mwenyewe nimemkubali.”+18 Ndiyo, maneno hayo tuliyasikia yakitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika ule mlima mtakatifu.