21 Tangu wakati huo, Yesu akaanza kuwafafanulia wanafunzi wake kwamba ni lazima aende Yerusalemu na kuteswa sana na wazee, wakuu wa makuhani, na waandishi, kisha atauawa, na siku ya tatu afufuliwe.+
24 Basi Pilato akaamua kutimiza dai lao. 25 Akamfungua yule mtu waliyemtaka, ambaye alikuwa amefungwa gerezani kwa sababu ya uchochezi na mauaji, lakini akamkabidhi Yesu mikononi mwao ili wamtendee wanavyopenda.