Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Mathayo 20:29-34
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 29 Walipokuwa wakitoka Yeriko umati mkubwa ukamfuata. 30 Na tazama! wanaume wawili vipofu waliokuwa wameketi kando ya barabara waliposikia kwamba Yesu anapitia hapo, wakapaza sauti: “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”*+ 31 Hata hivyo, umati ukawakemea na kuwaambia wanyamaze; lakini wakapaza sauti hata zaidi, wakisema: “Bwana, Mwana wa Daudi, tuhurumie!”* 32 Basi Yesu akasimama, akawaita na kuwauliza: “Mnataka niwafanyie nini?” 33 Wakamjibu: “Bwana, tunaomba macho yetu yafunguliwe.” 34 Yesu akawasikitikia, akayagusa macho yao,+ na mara moja wakaanza kuona, nao wakamfuata.

  • Luka 18:35-43
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 35 Yesu alipokaribia Yeriko kipofu mmoja alikuwa ameketi kando ya barabara akiombaomba.+ 36 Aliposikia umati ukipita, akaanza kuuliza kilichokuwa kikiendelea. 37 Wakamjibu: “Yesu Mnazareti ndiye anayepita!”⁠ 38 Ndipo akasema kwa sauti kubwa: “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!”* 39 Wale waliokuwa mbele wakaanza kumkemea wakimwambia anyamaze, lakini akazidi kusema kwa sauti kubwa: “Mwana wa Daudi, nihurumie!”* 40 Kisha Yesu akasimama na kuagiza mtu huyo aletwe kwake. Alipokaribia, Yesu akamuuliza: 41 “Unataka nikufanyie nini?” Akasema: “Bwana, naomba niweze kuona tena.” 42 Basi Yesu akamwambia: “Ona tena; imani yako imekuponya.”+ 43 Mara moja akaanza kuona tena, naye akaanza kumfuata Yesu+ huku akimtukuza Mungu. Pia, watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki