29 Ndipo wakatoka kwenye sinagogi na kwenda nyumbani kwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana.+ 30 Sasa mama mkwe wa Simoni+ alikuwa amelala akiugua homa, na mara moja wakamwambia Yesu kumhusu. 31 Yesu akamkaribia, akamshika mkono na kumwinua. Akapona homa, naye akaanza kuwahudumia.