Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Marko 1:29-34
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 29 Ndipo wakatoka kwenye sinagogi na kwenda nyumbani kwa Simoni na Andrea wakiwa na Yakobo na Yohana.+ 30 Sasa mama mkwe wa Simoni+ alikuwa amelala akiugua homa, na mara moja wakamwambia Yesu kumhusu. 31 Yesu akamkaribia, akamshika mkono na kumwinua. Akapona homa, naye akaanza kuwahudumia.

      32 Ilipofika jioni, jua lilipotua, watu wakaanza kumletea wote waliokuwa wagonjwa na waliokuwa na roho waovu;+ 33 na jiji lote lilikuwa limekusanyika mlangoni. 34 Basi akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa mbalimbali,+ akafukuza roho wengi waovu, lakini hakuwaruhusu hao roho waovu waseme, kwa maana walijua yeye ni Kristo.*

  • Luka 4:38-41
    Biblia Takatifu—Tafsiri ya Ulimwengu Mpya
    • 38 Alipotoka katika sinagogi akaenda nyumbani kwa Simoni. Mama mkwe wa Simoni alikuwa na homa kali, wakamwomba Yesu amponye.+ 39 Yesu akasimama kando yake, akaikemea ile homa, ikaisha. Papo hapo akasimama na kuanza kuwahudumia.

      40 Jua lilipokuwa likitua, wote waliokuwa na watu wenye magonjwa mbalimbali wakawaleta kwake. Akawaponya kwa kuweka mikono yake juu ya kila mgonjwa.+ 41 Roho waovu pia wakawatoka watu wengi, wakipaza sauti na kusema: “Wewe ndiye Mwana wa Mungu.”+ Lakini aliwakemea na hakuwaruhusu waseme,+ kwa maana walijua yeye ni Kristo.+

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki