25 “Suluhisha mambo upesi na mtu anayekushtaki, ukiwa naye njiani kwenda mahakamani, ili asikupeleke kwa hakimu, naye hakimu kwa mtumishi wa mahakama, nawe utupwe gerezani.+ 26 Hakika ninakuambia hutatoka humo mpaka utakapolipa sarafu yako ndogo ya mwisho.