6 Walipowakosa wakamkokota Yasoni na baadhi ya akina ndugu mpaka kwa watawala wa jiji, wakisema kwa sauti kubwa: “Watu hawa ambao wameipindua dunia inayokaliwa wako hapa pia,+ 7 naye Yasoni amewakaribisha. Watu hao wote wanapinga maagizo ya Kaisari, wakisema kuna mfalme mwingine, Yesu.”+