Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 3/8 uku. 20
  • Mwaka 1914— Kitenganishi cha Vipindi Viwili

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mwaka 1914— Kitenganishi cha Vipindi Viwili
  • Amkeni!—1990
  • Habari Zinazolingana
  • Ufalme wa Mungu Huanza Kutawala Katikati ya Adui Zake
    Kweli Iongozayo Kwenye Uzima wa Milele
  • Siku za Mwisho
    Kutoa Sababu kwa Kutumia Maandiko
  • Vita Ambayo Itavimaliza Vita
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1988
  • 1914-Mwaka Ulioshtua Ulimwengu
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1992
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1990
g90 3/8 uku. 20

Mwaka 1914— Kitenganishi cha Vipindi Viwili

KWA kuhesabu kuanzia kiangazi cha mwaka jana, ni miaka 75 ambayo imepita tangu risasi moja tu ya bunduki ilipozimisha uhai wa Ferdinand, Dyuki Mkuu wa Austria-Hangari. Wakati uo huo, ilianzisha mfululizo wa matukio yaliyotokeza vita iliyo ya kwanza katika tufe lote la sayari yetu—Julai 28, 1914.

Waandikaji na wanahistoria huelekeza kidole tena na tena kwenye vita hiyo ya kuogofya sana (na kwenye mwaka ambao iliwaka moto) kuwa ni kitenganishi cha vipindi viwili, hatua ya kugeukia, au mstari ulio kigawanyo katika historia ya kibinadamu. Je! kweli 1914 ulikuwa mwaka wa jinsi hiyo kwa jamii ya kibinadamu?

Angalia yale ambayo John Wilson aandika katika The Globe and Mail ya Toronto, Ontario, Kanada: “Vita ya Ulimwengu ya Kwanza yabaki ikiwa ndiyo alama ya kuonyesha mwanzo wa badiliko kuu katika historia ya ki-siku-hizi.” Ingawa masalio yaliyopo kuonyesha kulikuwako hilo pambano kali la duniani pote ni mahandaki ambayo yamemea nyasi, marisau yaliyoingia kutu, majengo ya ukumbusho, na nyanja zenye makaburi, Bw. Wilson aonelea kwamba kupita kwa muda mwingi tangu hapo hakujapunguza umaana wa kwamba mwaka 1914 ulikuwa kitenganishi cha vipindi viwili.

“Wazo la Kivictoria kuhusu mpigo wa hatua za kuelekea kuwa na ulimwengu ambao ungewezekana kuwa bora kuliko malimwengu yote liliangamia katika lile ogofyo baya sana lililoua watu milioni 10,” asema Wilson. “Mawazo ya leo ya elekeo la kutilia shaka na kupuuza mambo kabla ya kuyakubali yalitokana na ubatili na mabaya yaliyotokea Vimy na Flanders [kaskazini mwa Ufaransa na Ubelgiji]. Twaweza kuwa na uhusiano mzuri pamoja na wasichana wa ile miaka ya ishirini au wakulima waliopoteza makao yao ile miaka ya thelathini kwa urahisi kuliko ule tuwezao kuwa nao pamoja [na] wasitawisha-milki na watengeneza-maadili wa muda uliotangulia 1914. Ile Vita Kubwa ni kitenganishi cha vipindi viwili, . . . ng’ambo ile nyingine ikiwa na kipindi kigeni chenye kurudi nyuma katika historia.”

Lakini yaliyotukia tangu mwaka 1914 ndiyo huthibitisha hali ya mwaka huo ya kuwa kitenganishi cha vipindi viwili. Mbali na kuwa ndiyo “vita ya kumaliza vita vyote” kama ilivyokusudiwa kuwa, jambo lile tu ambalo Vita ya Ulimwengu 1 ilifanya ni kuuingiza ulimwengu katika aina mpya ya vita. Kutokana na makaa machache yaliyobakizwa nayo, kukatokea moto mkali wa Vita ya Ulimwengu 2. Miaka 50 iliyopita, siku ya Septemba 1, 1939, Ujeremani ilivamia Polandi, na vita ya ulimwengu ya pili ikaanza. Ikiua kufikia watu milioni 55, kwa kweli iliizidi mno Vita ya Ulimwengu 1 na kuanzisha hofu zilizo mpya, zenye kuogofya sana hisia za kibinadamu; wala haikuleta mwisho wa vita. Tangu 1945 vita kama 150 vimeua karibu watu milioni 20!

Katika 1914 jamii ya kibinadamu iliingia katika muda wa huzuni kubwa. Kama vile mwandikaji Wilson asemavyo: “Mtu hufikiri sana akumbukapo kwamba, kwa sababu ya maogofyo yote yaliyotoka kwenye mahandaki, jamii ya watu baada ya 1918 ilihangaikia kuzika wafu wakiwa wamepangwa katika mistari yenye utaratibu na kujengewa vitu vya kuwakumbuka. Sisi twaishi chini ya tisho la uharibifu wa duniani pote ulio mkubwa kwa kadiri isiyoweza kuwaziwa na askari waliomiminika mbio katika Mwinuko wa Vimy. Kukiwa na vita nyingine ya ulimwengu, ni nani atajenga vitu vya kuwakumbuka wafu watakaouawa nayo?”

Muda mrefu kabla ya 1914, Wanafunzi wa Biblia walio waaminifu (kama vile Mashahidi wa Yehova walivyojulikana wakati huo) walikuwa tayari wakielekeza mbele kwenye mwaka huo kuwa kitenganishi cha vipindi viwili katika historia ya kibinadamu. Kulingana na tarehe za matukio ya Biblia zilizo za kutegemeka zaidi, mfumo huu mzima wa mambo ya ulimwengu uliingia katika awamu mpya katika 1914, kile kipindi chenye kufikia upeo ambacho charejezewa na Biblia kuwa “siku za mwisho.”—2 Timotheo 3:1-5; Mathayo 24:1-14.

Hata hivyo, Biblia yakitia alama kipindi hiki cha “siku za mwisho” kuwa ni zaidi ya wakati wa taabu. Pia ni wakati wa tumaini. Mbali na kuruhusu mwanadamu ajiharibu mwenyewe katika vita ya mwisho ya ulimwengu, Mungu aahidi kuchukua hatua na kufanya vita dhidi ya wote ambao huijaza dunia jeuri. Wakati huo silaha zote za vita zitaharibiwa daima. Kuanzia hapo na kuendelea, aina ya binadamu yote itajifunza njia za amani, si vita. (Isaya 2:2-4; Luka 21:28; Ufunuo 16:14) Lo, ni badiliko lililoje! Hakika, hicho kitakuwa ndicho kitenganishi chenye badiliko kubwa zaidi katika vipindi vya historia yote ya kibinadamu.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki