Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g90 5/8 uku. 30
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1990
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • UPUNGUFU WA MAKASISI WENYE KUSTAHILI
  • UKUZI WA MASHAHIDI WAWATIA WASIWASI WAKATOLIKI WA ITALIA
  • JITU LENYE KUTOWEKA
  • UHITAJI WA BIBLIA
  • KUZAA WATOTO KWA URAHISI ZAIDI
  • UTUMISHI MPYA WA SIMU
  • KIELELEZO KIBAYA
  • NYWELE ZA UASI
  • KUZUIA MIMWAGIKO YA MAFUTA
  • UHODARI WA KUPIGA PICHA
  • Je, Ninahitaji Simu ya Mkononi?
    Amkeni!—2002
  • Sanduku La Swali
    Huduma ya Ufalme—2013
Amkeni!—1990
g90 5/8 uku. 30

Kuutazama Ulimwengu

UPUNGUFU WA MAKASISI WENYE KUSTAHILI

“Viongozi Waprotestanti, Waroma Wakatoliki na Wayahudi pia wasumbuliwa-sumbuliwa na takwa la kudumisha hesabu na ubora wa makasisi wao,” laripoti The New York Times. “Jambo lenye kutatanisha hali hiyo ni utofautiano ambao viongozi waona wawezekana kuwa kati ya mahitaji ya kanisa na mandharinyuma na miradi ya wengi wenye hamu ya kuwa makasisi.” Leo wanaseminari wasemwa kuwa “tofauti kabisa” na wale wa miaka 25 tu iliyopita. Katika seminari za Kiprotestanti, asilimia kubwa zaidi ya wale ambao sasa wanatafuta ukasisi ni wanawake. Na kwa kuwa kuna waombaji wachache zaidi, seminari zimekuwa chini ya msongo wa kushusha viwango vya elimu na kukubali wanafunzi wengi zaidi wasiofaa sana. Warasimu Wakatoliki wamekuwa wakihangaika juu ya mitazamo ya wanaseminari kuhusu ngono na juu ya vile upadri “unavutia hesabu kubwa isivyo kawaida ya wataka ukasisi walio wagoni-jinsia-moja.” Ripoti hiyo yaongezea hivi: “Tofauti moja kati ya wanaseminari wa leo na watangulizi wao yaonekana kuwa ya kweli bila kujali wana imani au madhehebu, jinsia na umri gani: Hawana msingi ulio imara sana katika pokeo lao la kidini.”

UKUZI WA MASHAHIDI WAWATIA WASIWASI WAKATOLIKI WA ITALIA

“Maonyo juu ya Mashahidi wa Yehova yamekuwa kichwahabari chenye kutajwa mara nyingi katika parokia fulani za Roma,” lasema The Catholic Standard and Times. “Jambo lenye kuhangaisha Kanisa ni kadiri ya ukuzi wa Mashahidi na mbinu zao za kutumia nishati nyingi na zenye kuonekana kuwa zenye mafanikio za kuingiza wafuasi wapya.” Mapema kidogo mwakani, profesa wa seminari Monsinya Lorenzo Minuti alimwambia Papa John Paul 2 “kwamba Mashahidi wa Yehova ni ‘mafuko’ wanaofukua Kanisa na akawalinganisha na ‘kipuku.’” Aliomba kanisa lichukue hatua za uzuizi, kana kwamba linakomesha tauni. Kulingana na Minuti, hesabu ya Majumba ya Ufalme katika Roma iliongezeka kutoka 10 katika 1982 hadi 66 katika 1989, hali kuna mahekalu na makanisa 44 tu kwa watu wengine wote wasio Wakatoliki jijini. “Siri ya fanikio la Mashahidi katika bara la mapapa na makanisa ni bidii yao ya kueneza evanjeli,” karatasi-habari hiyo ikasema, ikitoa wito wa “kazi mpya ya Kikatoliki ya kueneza evanjeli Italia.”

JITU LENYE KUTOWEKA

Nyangumi wa buluu angali hajatoka taabani. Ni wachache sana waliobaki kuliko vile wanasayansi walivyotumainia. Uwindaji wote wa nyangumi wa buluu ulipigwa marufuku nyuma huko katika 1966, lakini yeye haachi kukaribia ukingo wa kutokomea kabisa. Kabla ya siku zile za kuwinda nyangumi kibiashara, walikuwako wengi kufikia 225,000. Wanasayansi walikuwa wakitumaini kwamba wenye kubaki walikuwa kuanzia 11,000 hadi 14,000. Lakini matokeo ya kwanza kutokana na uhesabu wa moja kwa moja yalidokeza kwamba huenda kukawa na wachache kuliko 1,200 au 1,500. Nyangumi hao majitu, ambao hukua kufikia urefu wa meta 31 na wana uzani wa kufikia tani 150—karibu kulingana na kundi la ndovu 30—waweza hata kuwa ndio viumbe wakubwa zaidi waliopata kuikaa dunia. Wao hunyonyesha wachanga wao kwa mwaka mmoja, huchukua miaka sita kukomaa, na huzaa mara moja tu katika miaka miwili. Hivyo, wao huongezeka polepole baada ya kupunguka. Lakini uwindaji haramu huenda ukawa pia ni kisababishi cha hesabu zao ndogo.

UHITAJI WA BIBLIA

Uhitaji wa Biblia katika Urusi umekuwa ukiongezeka, na kujapokuwako shehena zenye nakala milioni mbili katika muda wa miezi 18, uhitaji waendelea kuwapo bila kupungua. Kama ilivyoripotiwa katika Church Times ya London, “biblia zaidi ziliingizwa katika Urusi wakati wa 1988 kuliko katika kipindi kizima cha tangu yale Mapinduzi Makubwa ya 1917.” Kwa kutofautiana na miaka ya mapema kidogo, hati za kuruhusu uingizaji zimekubaliwa tayari kwa ajili ya shehena za ziada kutoka United Bible Societies.

KUZAA WATOTO KWA URAHISI ZAIDI

Wanawake watazaa watoto kwa urahisi zaidi wakichuchumaa, ndivyo wasema wazalishaji katika Uingereza. Uchunguzi uliofanywa juu ya visa kama 400 vya kujifungua umeonyesha kwamba wanawake walio wengi wenye kuzaa huwa na utendaji mzuri zaidi wakiwa katika mkao wima kuliko wakiwa katika mkao wa kubetuka (kuinama). Uchunguzi huo ulipata kwamba mchuchumao uliotegemezwa huruhusu kuwe na msukumo imara zaidi na wenye matokeo zaidi, hivyo ukipunguza sana urefu wa ile hatua ya pili ya kujifungua na uhitaji wa kutumia vibano. Sasa vitegemezo viwili vyatumiwa, viti vya uzazi na matakia ya uzazi. Dakt. Jason Gardosi wa Hospitali Kuu ya Milton Keynes katika Buckinghamshire, Uingereza, aliyeongoza uchunguzi huo, apendekeza utumizi wa takia, kwa maana waweza kuwekwa moja kwa moja juu ya kitanda na hufanya kujifungua kuwe rahisi zaidi kwa kuruhusu mifupa ya nyonga ipanuke zaidi. Kati ya wanawake wenye kutumia chombo hicho, asilimia 95 walisema wangetumia tena mkao wa kuchuchumaa kwa uzazi wao ufuatao. Kwa kupendeza, huu ndio mkao ambao hurejezewa katika Biblia kwenye Kutoka 1:16, NW.

UTUMISHI MPYA WA SIMU

Simu zenye kumbukumbu, zilizoundwa kujipiga nambari zitakiwazo, zisizoendeshwa kwa mikono, na zenye mahali pa kuonyesha tarakimu, na mambo mengineyo, zimekuwa jambo la kikawaida. Lakini bado hizo hulia wakati tu wito wa mpiga-simu uingiapo. Sasa hilo linabadilika. Wakati kampuni za simu katika United States ziwekapo vifaa vipya vya kutoa ishara, zinatoa toleo la utumishi mpya mwingi ambao simu itafanya ukibonyeza tu vifungo kadhaa. Vyenye kutiwa ndani ni: kufuatisha nambari ya simu—hii huunga nambari ya mpiga simu pamoja na kampuni ya simu hata ikiwa wito wa mpiga-simu ulikuwa mfupi sana naye ameweka simu chini; fungu la nambari—nambari ambazo tayari zimepangiliwa katika simu husikia ujumbe wa kwamba sasa hivi wewe huchukui simu zenye kupigwa; mpigo wa kurudia—kwa dakika 30 hujaribu nambari yenye shughuli nyingi huku ikikuruhusu bado upige au upokee miito mingine ya simu; mpigo wa kurudishwa—ikiwa simu yaacha kulia wakati tu unapofika mahali ilipo, utendaji huu hupiga namba ya mtu wa mwisho aliyekuwa akijaribu kukupasha habari; mpigo wenye umuhimu wa kwanza—hutoa mlio mpambanufu wakati simu ipokewapo kutoka nambari fulani-fulani; ID (Kitambulisho) ya mpiga-simu—huonyesha katika chombo chenye kioo cha kuonyesha nambari ya mwenye kupiga simu.

KIELELEZO KIBAYA

Ingawa watoto huiga watu wazima kwa kuigiza vituko vya kinyumbani au vya udaktari, polisi waligutuka katika Lebanoni, Pennsylvania, walipogundua kibanda katika uwanja wa michezo ambako watoto walikuwa wakitumia ua bandia wa dawa za kulevya, wakitumia mifuko ya sukari na vibano vya nyasi. Kandokando ya hizo dawa za bandia, zilizosemwa kuwa zilitoka kwa mvulana wa miaka saba na msichana wa miaka tisa, palikuwa na daftari ya mikataba ya kuuziana dawa za kulevya na kipande cha kudai deni. Hati moja ilisomeka hivi: “Kokeni, nusu-mfuko mdogo, senti 55 [za U.S.], mifuko midogo, dola 1.” Watoto wanaiga kielelezo cha wazazi wao, akasema kachero Robert Bowman, Jr. “Wanataka kupata pesa nyingi bila kufanya kazi.”

NYWELE ZA UASI

New York na Los Angeles zimeanzilisha mtindo mwingine wa nywele: kukaribia kunyolewa upara kwa kutiatia vigezo vya namna mbalimbali. Mitindo-kisanaa imetia ndani umbo la jinsi ghorofa za Jiji la New York huonekana angani, umbo la Golden Gate Bridge, na maneno ya kampuni yenye kuonekana kuwa maarufu. Kulingana na The Wall Street Journal, sinema moja ilisaidia kufanya namna-mtindo huo uwe maarufu kwa sababu mwigizaji mmoja mashuhuri alikuwa na kigezo cha kunyolewa michoro ya radi katika nywele yake. Kuhusu kwa nini namna-mtindo huo wa nywele ulichaguliwa, Journal yanukuu mkurugenzi wa sinema hiyo kuwa akisema hivi: “Tulikuwa tukijaribu kupata jambo fulani la kuonyesha roho ya uasi.”

KUZUIA MIMWAGIKO YA MAFUTA

Dokezo moja la kupunguza mimwagiko ya mafuta ni kujenga melimafuta zenye bodi maradufu. Lakini hiyo yapunguza nafasi ya shehena na, bodi ikipasuka, haitazuia mafuta kutoka. Serikali ya Kiswedi yadokeza kwamba njia bora zaidi ni “njia ya kuacha nafasi wazi” katika muundo wa tangi. Kama ilivyoelezwa katika The Economist, hiyo hutumia kanuni ya kubana hewa ibakie mahali pamoja ili kuyashikilia mafuta. Kielelezo sahili ni hiki: Nyonya umajimaji uuvute kuja juu nusu ya mrija wa kuvutia, halafu ufinye ncha ya juu. Umajimaji hautatoka hapo mpaka uuachilie. Wahandisi Waswedi walisababu kwamba ikiwa nafasi wazi iliyo upande wa juu wa ngama yaweza kufungwa barabara isiingiwe na hewa, hakuna mafuta ambayo yangemwagika tundu likitokea chini. Walipendekeza kukalafati ngama kabisa lakini kuacha wazi vali fulani. Halafu, aksidenti ikitukia, hewa ingeweza kutolewa nje katika vali hizi ili kushusha msongo uliomo na kufanya ngama ifungike isiingiwe na hewa. Kufikia sasa, yasema The Economist, pendekezo hilo limepuuzwa, na njia hiyo yabaki bila kutahiniwa.

UHODARI WA KUPIGA PICHA

Wakati chomboanga Voyager 2 kiliporudisha picha wazi zenye maelezo marefu kuhusu Neptune, ambayo kwa sasa ndiyo sayari iliyo mbali zaidi kutoka kwenye jua, wabuni wacho waliingiwa na furaha ya kiwewe. Katika safari yayo ya kwanza ya kilometa milioni elfu 7, chomboanga kidogo hicho cha tani moja kiliitumia fursa nzuri ya mpangilio sawia wa sayari ambao hutukia mara moja tu kila miaka 176. Kwa mfuatano, kwanza kilizuru Jupiter, Saturn, na Uranus, kikirudisha habari kutoka vyombo vyayo 11 vya kisayansi, kutia na kamera mbili za televisheni. Uhodari wa kupeleka picha bora sana za Neptune na miezi yayo kikiwa kwenye umbali wa karibu kilometa milioni elfu kutoka duniani haukuwa jambo rahisi. Nurujua huko ni kidogo sana huko kwa kadiri ya sehemu moja kwa elfu ya uangavu ambao huangukia dunia, hiyo ikifanya iwe lazima kamera zifunguliwe wazi kwa muda mrefu na kuzungushwa-zungushwa ili kuzuia picha zisitoke zikiwa nyeusi. Wakati ishara ya kutoka kwenye transmita ya wati 20 ya Voyager ilipofikia vituo vya duniani vya kuangalia usafirianga, ilikuwa imefifia ikawa chini ya wati moja kwa upungufu wa milioni elfu moja na kuchangamana na kelele ya angani yenye kuhisiwa kwa kutumia sumakumeme.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki