Ni Lugha Ipi Inayosemwa Zaidi?
Ikiwa unafikiria hilo kwa habari ya lugha ya kimataifa iliyo maarufu zaidi, yaelekea jibu lako kwa swali hilo litakuwa ni “Kiingereza.” Hata hivyo, kulingana na World Almanac and Book of Facts cha 1990, Kichina cha Mandarin, kinachosemwa na watu wapatao milioni 844, ndicho lugha inayotumiwa zaidi na familia ya kibinadamu. Kwa kulinganisha ni milioni 437, waliosambaa ulimwenguni pote, wanaosema Kiingereza. Unafikiri ni lugha gani ambayo ingekuwa ya tatu katika kundi hilo la ulimwengu? Kifaransa au Kihispania? La. Ni Kihindi, kinachosemwa na watu milioni 338, hasa katika India. Kihindi na Kiurdu, ambazo husemwa na milioni 90, hasa katika Pakistan, “kwa ujumla ni lugha ile ile, Kihindustani,” kulingana na kichapo icho hicho.