Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g92 4/8 uku. 20
  • “Si Kosa Langu!” Muhula wa Kutoa Udhuru

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • “Si Kosa Langu!” Muhula wa Kutoa Udhuru
  • Amkeni!—1992
  • Habari Zinazolingana
  • Je, Biblia Inaweza Kukusaidia Kushinda Uraibu wa Dawa za Kulevya?
    Habari Zaidi
  • Ni Nani Hupatwa na Uzoelevu, na kwa Nini?
    Amkeni!—1994
  • “Naitaka Sasa!” Muhula wa Utoshelezo wa Papo Hapo
    Amkeni!—1991
  • Utendaji Unapokuwa Uzoelevu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1992
g92 4/8 uku. 20

“Si Kosa Langu!” Muhula wa Kutoa Udhuru

PUU! Mama ya Johnny mchanga akimbia ndani jikoni aweze kuona kile kilichosababisha mlio huo wa kuogofya. Huko, chupa ya kuwekea biskuti imevunjika-vunjika sakafuni. Johnny amesimama hapo, huku akishika biskuti kilegevu kwa mkono wake na akajaribu kuonekana asiye na hatia wakati ule ule. “Halikuwa kosa langu!” yeye asema kwa ghafula.

WAZAZI wanajua vizuri sana kwamba watoto wana tatizo la kukubali daraka la makosa yao wenyewe. Lakini jamii ya watu wazima leo wana tatizo hilo hilo. Watu wengi zaidi na zaidi ni kama wanaamini kwamba tamaa yao ya kujitosheleza wenyewe ni nyingi kwa kadiri ambavyo hawawezi kutarajiwa kuikinza.

Kwa mfano, fikiria yule mtu aliyenajisi mwanamke yule yule mmoja mara tatu. Alijitetea wakati wa kusikilizwa kwa kesi yake kwamba yeye alikuwa anasumbuliwa na hormoni zake za kiume; alikuwa na kiwango cha juu sana cha hormoni za shahawa katika mapumbu. Mtu huyo aliachiliwa huru. Mwanasiasa aliyepatikana akidanganya alitoa udhuru wa kukiuka sheria kuwa tatizo la kileo. Mlanguzi mwenye kuingiza nchini dawa za kulevya aliachiliwa huru baada ya yeye kudai kwamba ‘alikuwa akiugua tamaa ya dawa za kulevya.’

Kulingana na U.S. News & World Report, vikundi zaidi ya 2,000 hukutana kila juma ili kushauri wale ambao hujiona kuwa wazoevu wa ngono au mahaba. Mashirika ya kitaifa zaidi ya 200 yamejiunga kuwa vyama vinavyosaidia Walevi Wasiotajwa Majina ili yasaidie “wanaosumbuliwa” na “mazoevu” mengine, kama vile Wapiga-Wake Wasiotajwa Majina, Walawiti Walafi Wasiotajwa Majina, Wanakamari Wasiotajwa Majina, Wadeni Wasiotajwa Majina, Wazembe Wasiotajwa Majina, na Walewa-Kazi Wasiotajwa Majina.

Wastadi wengine hukubali wazo la kwamba namna hizo zote za tabia mbovu huenda zikawa zenye uzoevu, lakini wengine hushangazwa na mtindo huo mpya wa uzoevu. Ni kama vile mwanasaikolojia mmoja alivyoeleza wazo hilo: “Kuumba ulimwengu ambao una maradhi ya uzoevu kwaweza kumaanisha kuumba ulimwengu ambao kila kitu kinaruhusiwa.” Daktari mmoja wa akili atahadharisha kwamba mara tu watu waanzapo kujiita wanaswa hoi katika uzoevu fulani, wanakuwa wagumu zaidi kutibika; udhuru wao unakuwa sehemu ya utambulisho wao.

Dakt. William Lee Wilbanks, profesa wa hukumu ya mhalifu, akazia kwamba mtindo wa kisasa wa kutoa udhuru kwa uzoevu ni sehemu ya falsafa yenye maneno manne ambayo aiita Uchafu Mpya: “Mimi siwezi kujisaidia mwenyewe.” Yeye ashutumu “mwelekeo unaoongezeka katika jamii ya kisayansi wa kuona wanadamu kama vyombo vinavyochochewa na nguvu zitokazo nje au ndani yao wasizoweza kudhibiti.” “Oni hilo,” yeye aongezea, “ladokeza kwamba pendezi la hiari linahusika kidogo sana au halihusiki hata kidogo katika tabia ya kibinadamu.”

Uchunguzi mbalimbali umedokeza kwamba pendezi la kibinadamu huenda likawa na uvutio zaidi kushinda hata mazoevu ya zamani kuliko vile imedhaniwa. Kwa mfano, karibu asilimia 75 ya wazoevu wa heroini hushindwa katika jitihada zao za kuwacha tabia ya kuitumia. Lakini miongoni mwa wakale wa Vita ya Vietnam, ufanisi wa kuwacha dawa hiyo ni wa juu sana—karibu asilimia 90 wanaweza kuwacha. Kwa nini? Dawa ni ile ile, hali yake ya uzoevu ni ile ile. Je! ingeweza kuwa, kama adokezavyo Wilbanks, kwamba “thamani yao na nidhamu ya kibinafsi ziliwasaidia ‘Kusema La’”? Si kwamba utegemeaji wa kemikali au hata tabia ya tangu kuzaliwa kuelekea matatizo fulani si halisi. Kama vile Wilbanks anavyosema, mambo hayo “yaweza kufanya vita dhidi ya ushawishi kuwa ngumu zaidi. Lakini vita hiyo bado yaweza kushindwa.”

Ni kweli yaweza. Shawishi la utoshelezo wa papo hapo linaweza kuwa na nguvu sana, lakini halina nguvu zote kabisa. Kama vile kazi ya Mashahidi wa Yehova imeonyesha ulimwenguni pote, wazoevu wa dawa za kulevya, walevi, wazinzi, wacheza-kamari, na wagoni-jinsia-moja si lazima wapate utoshelezo wa tamaa zao. Kwa kutumia uwezo wao wa kuchagua na, la maana zaidi, msaada wa roho takatifu ya Mungu, wanaweza na huweza kushinda matatizo yao. Hivyo, hata “wastadi” waseme nini, Muumba wetu ajua tunapokuwa na daraka kwa matendo yetu. (Hesabu 15:30, 31; 1 Wakorintho 6:9-11) Lakini yeye ni mwenye rehema pia. Hatazamii kwetu mambo mengi kupita kiasi, ‘akikumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi.’—Zaburi 103:14.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki