Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g94 4/22 kur. 3-5
  • Ni Nani Hupatwa na Uzoelevu, na kwa Nini?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Ni Nani Hupatwa na Uzoelevu, na kwa Nini?
  • Amkeni!—1994
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Dawa za Kulevya na Kileo
  • Matatizo ya Ulaji
  • Je, Biblia Inaweza Kukusaidia Kushinda Uraibu wa Dawa za Kulevya?
    Habari Zaidi
  • Nini Ikiwa Mzazi Wangu ni Mraibu wa Dawa za Kulevya au Pombe?
    Maswali Ambayo Vijana Huuliza—Majibu Yafanyayo Kazi, Buku la 2
  • Kushinda Uzoelevu wa Vitu
    Amkeni!—1994
  • Utendaji Unapokuwa Uzoelevu
    Amkeni!—1994
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1994
g94 4/22 kur. 3-5

Ni Nani Hupatwa na Uzoelevu, na kwa Nini?

UENDESHAPO gari lako katika barabara kuu, kisha unasikia sauti fulani isiyo ya kawaida ya kutatarisha ikitoka kwenye injini ya gari lako. Utafanya nini? Je! utachunguza injini ili ujue tatizo hilo? Au utaongeza tu sauti ya redio ya gari lako ili usisikie sauti inayotoka kwenye injini?

Jibu ni wazi, lakini nyakati zote wazoelevu hufanya uchaguzi mbaya—si kwa magari yao, bali kwa maisha zao. Kwa kuwa wazoelevu wa vitu kama dawa za kulevya, kileo, na hata chakula, wengi hujaribu kusahau matatizo yao binafsi badala ya kujaribu kukabiliana nayo kwa mafanikio.

Mtu aweza kujuaje kama amekuwa mzoelevu? Daktari mmoja asema hivi: “Kwa msingi, matumizi ya dawa au utendaji fulani ni uzoelevu ikiwa unakutokezea matatizo maishani mwako lakini bado unaendelea nao tu.”

Hali ikiwa hivyo, basi mara nyingi kuna tatizo baya zaidi ndani yako mwenyewe linalohitaji kuchunguzwa kabla ya tabia ya kuwa mzoelevu kubadilishwa.

Dawa za Kulevya na Kileo

Ni nini hufanya mtu aanze kuwa mzoelevu wa dawa za kulevya na kileo? Mara nyingi mbano wa marika na udadisi husababisha uzoelevu sana, hasa miongoni mwa vijana. Kwa kweli, sababu inayofanya watu wengi wawe wazoelevu ni mashirika yao mabaya pamoja na wale wanaotumia vibaya kileo na dawa za kulevya. (1 Wakorintho 15:33) Huenda hiyo ikaeleza sababu ya matokeo ya uchunguzi wa U.S. uliogundua kwamba asilimia 41 ya wanafunzi wanaoendelea kumaliza shule za sekondari hunywa pombe kupindukia kila baada ya majuma mawili.

Lakini kuna tofauti kati ya matumizi mabaya na uzoelevu. Watu wengi watumiao vibaya vitu fulani si wazoelevu.a Watu hao wanaweza kuacha kutumia vibaya vitu hivyo na wasihisi mkazo wa kurudia vitendo vyao. Lakini wazoelevu hupata kwamba hawawezi kuacha vitendo vyao. Na zaidi, raha yoyote waliyokuwa wakipata huondolewa na kihoro. Kitabu Addictions chaeleza hivi: “Kwa kawaida wazoelevu hufikia hatua fulani ambayo wao huanza kujichukia, na kuanza kusononeka sana juu ya jinsi ambavyo wameshindwa na uzoelevu wao.”

Watu wengi wanaotegemea kileo au dawa za kulevya huzitumia kuwa njia ya kuepuka matatizo ya kihisia-moyo. Matatizo kama hayo ni mengi sana siku hizi. Na tusishangae sana, kwani Biblia yatambulisha siku hizi kuwa “siku za mwisho” za mfumo huu wa mambo, wakati ambapo kungekuwako “nyakati za hatari.” Biblia ilitabiri kwamba watu wangekuwa “wenye kupenda fedha,” “wenye kiburi,” “wasio waaminifu-washikamanifu,” [New World Translation], “wakali,” “wasaliti,” na “wenye kujivuna.” (2 Timotheo 3:1-4) Tabia hizo zimetokeza hali zinazoleta uzoelevu.

Matatizo ya kihisia-moyo ya Susan yalitokea kwa sababu alitendwa vibaya wakati uliopita. Kwa hiyo, alianza kutumia kokeini. “Ilinipa hisi bandia ya kujidhibiti na kujistahi,” asema. “Ilinipa hisi ya kuwa na uwezo ambao sikuwa nao katika maisha yangu ya kawaida.”

Uchunguzi mmoja wa vijana wa kiume wazoelevu ulifunua kwamba zaidi ya vijana theluthi moja kati yao walikuwa wametendwa vibaya kimwili. Uchunguzi mwingine wa wanawake wazima 178 wazoelevu uligundua kwamba asilimia 88 kati yao walikuwa wametendwa vibaya sana kwa njia moja au nyingine. Biblia katika Mhubiri 7:7 yasema hivi: “Jeuri humpumbaza mwenye hekima.” Mtu anayeugua kihisia-moyo kwa sababu ya kupatwa na mambo mabaya sana maishani huenda baadaye akaanza kutumia dawa za kulevya au kileo kipumbavu ili apate kitulizo.

Lakini dawa za kulevya na kileo si vitu pekee vyenye kutokeza uzoelevu.

Matatizo ya Ulaji

Matatizo ya ulaji (ambayo wastadi fulani huita uzoelevu), nyakati nyingine hutumika kuwa njia ya kuepuka hisia mbaya. Mathalani, watu wengine hutumia uzito wa kupita kiasi kuwa udhuru wa kutamauka kwao. “Nyakati nyingine nafikiri mimi hubaki nikiwa mnene kwa sababu kila kitu kibaya kitokeacho maishani mwangu husababishwa na kunenepa kwangu,” asema Jennie. “Kwa sababu mimi ni mnene, ikiwa mtu yeyote hanipendi, naweza tu kusema ni kwa sababu ya unene wangu.”

Kwa watu wengine, chakula huandaa hisi bandia ya kujidhibiti.b Huenda chakula kikawa eneo la pekee ambalo mtu ahisi ana uwezo fulani. Watu wengi wenye matatizo ya ulaji hufikiri kwamba wamepungukiwa kwa njia fulani. Ili kuwa na hisia za kujistahi, wao hujaribu kudhibiti tamaa ya mwili wao ya kutaka chakula. Mwanamke mmoja alisema hivi: “Wafanyiza utawala katika mwili wako mwenyewe, ambamo wewe mwenyewe ndiye mtawala mkatili, mtawala mwenye mamlaka yote.”

Maono yaliyotajwa hapo juu hayaelezi sababu zote za uzoelevu wa dawa za kulevya, kileo, na chakula. Kuna sababu nyinginezo zinazohusika. Wastadi fulani hata hudokeza kwamba kuna sababu za urithi zinazofanya wengine wawe wazoelevu kwa urahisi zaidi ya wengine. “Jambo tuonalo ni mchanganyiko wa utu, mazingira, biolojia na hali ya kukubaliwa katika jamii,” asema Jack Henningfield wa Taasisi ya Kitaifa ya Matumizi ya Dawa za Kulevya. “Hatutaki kudanganyika kwa kutazama sababu moja tu.”

Hali iwe ni nini, hakuna mzoelevu yeyote—hata uzoelevu wake uwe umetokana na nini—anayeelekea kuangamia kimwili au kihisia moyo. Kuna msaada.

[Maelezo ya Chini]

a Bila shaka, matumizi mabaya ya kileo au dawa nyinginezo za kulevya—yawe yanatokeza uzoelevu ama sivyo—yachafua na ni lazima yaepukwe na Wakristo.—2 Wakorintho 7:1.

b Habari za ziada za ulaji wa kupita kiasi zaweza kupatikana katika matoleo ya Kiingereza ya Amkeni! ya Desemba 22, 1990, na Februari 22, 1992.

[Sanduku katika ukurasa wa 5]

Mweneo wa Ulimwenguni Pote wa Uzoelevu

◼ Uchunguzi mmoja katika Meksiko ulifunua kwamba kila mtu 1 kati ya 8 wenye umri wa kati ya miaka 14 na 65 ni mzoelevu wa kileo.

◼ Mfanyakazi wa jamii Sarita Broden aripoti kwamba kuna mweneo mkubwa wa matatizo ya ulaji katika Japani. Yeye asema hivi: “Kati ya miaka 1940 na 1965, matatizo ya ulaji yameongezeka hatua kwa hatua yakifuatwa na ongezeko kubwa la wagonjwa wanaolazwa hospitalini na wale wanaoruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kutibiwa kati ya miaka 1965 na 1981. Hata hivyo, tangu 1981 kumekuwa na ongezeko la kustaajabisha la ugonjwa wa hangaiko la kuwa mnene mno na ugonjwa wa bulimia.”

◼ Nchini Uchina idadi ya watumiaji wa heroini yaonekana inaongezeka haraka sana. Dakt. Li Jianhua, anayefanya kazi katika Kituo cha Utafiti cha Matumizi ya Dawa za Kulevya cha Kunmig, asema: “Heroini imeenea kutoka mpakani mwa Uchina hadi sehemu za ndani za nchi hiyo, kutoka sehemu za mashambani hadi majijini na kutumiwa na vijana na hata vijana wachanga zaidi.”

◼ Katika Zurich, Uswisi, mpango wa kununua na kuuza dawa za kulevya waziwazi haukufaulu. “Tulifikiri tungegundua walanguzi wa dawa za kulevya, lakini tulishindwa,” asema Dakt. Albert Weittstein, akilalamika kwamba kumbe walikuwa wakiwavutia walanguzi na watumiaji wa dawa za kulevya kutoka sehemu za mbali.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki