Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 1/8 uku. 32
  • Uvumilio wa Kidini—Miaka 500 Baadaye!

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Uvumilio wa Kidini—Miaka 500 Baadaye!
  • Amkeni!—1993
Amkeni!—1993
g93 1/8 uku. 32

Uvumilio wa Kidini—Miaka 500 Baadaye!

MIAKA mia tano iliyopita, Christopher Columbus aliabiri kutoka Uhispania. Siku moja tu kabla Columbus hajaondoka, meli nyingine ziliondoka Uhispania, zikielekea upande tofauti. Columbus na watu wake walirudi kwa ushindi, wakiwa wamegundua nchi mpya. Lakini wale wasafiri wengine wasiofanikiwa hawangeona tena nchi yao.

Watu hao walikuwa akina nani, na kwa nini walifukuzwa kutoka nchi yao? Wao walikuwa Wayahudi Wahispania. Majuma mawili kabla Columbus hajapokea kibali cha mfalme kwa safari yake ya uvumbuzi, Ferdinand na Isabella, watawala Wakatoliki wa Uhispania, walitoa sheria ya kufukuza Wayahudi wote wa Uhispania, “wasirudi tena kamwe.” Waliwashtaki Wayahudi wa Uhispania juu ya kuhalifu imani takatifu ya Kikatoliki.

Sheria hiyo, pamoja na Baraza la Kuwahukumu Wazushi wa Kidini lililokuwa limeanzishwa karibuni, ilitia alama mwanzo wa krusedi za kufanya Uhispania iwe ya Wakatoliki tu. Mwongo mmoja baada ya kufukuzwa kwa Wayahudi, Wamoori wowote waliofuata imani ya Kiislamu walifukuzwa pia. Na upesi Baraza la Kuhukumu Wazushi wa Kidini likaondolea mbali vikundi vya Kiprotestanti vilivyokuwa vikijianzisha. Columbus, akiunga mkono ile roho ya kutovumilia ya watawala wake, alisema juu ya kutotia ndani Wayahudi katika nchi zozote ambazo angevumbua.

Ile roho ya kutovumilia kwa kidini katika Uhispania iliendelea, hata kufikia karne hii. Chini ya udikteta wa Francisco Franco, dini ya Katoliki tu ndiyo iliyofurahia “ulinzi rasmi.” Wengi waliotaka kufuata imani nyingine walikamatwa bila sababu. Mashahidi wa Yehova katika Uhispania walifungwa gerezani kwa shtaka la kuudhi umoja wa kiroho wa Uhispania. Katika 1959 waziri wa serikali Camilo Alonso Vega aliagiza polisi “waangamize kabisa” utendaji wa Mashahidi. Lakini kwa furaha, nyakati zimebadilika.

Mnamo Machi 31, 1992, miaka mia tano barabara baada ya wale waliomtangulia kutia sahihi sheria iliyofukuzia mbali Wayahudi, Juan Carlos, mfalme wa sasa wa Uhispania, alizuru sinagogi la Madrid katika mkutano wenye kutia alama wa Wakuu wa Uhispania na wazao wa wale Wayahudi Wahispania waliotoroshwa.

“Tumefunga ukurasa wa kutovumilia katika Uhispania,” akajulisha waziri wa sheria wa Uhispania, Tomás de la Quadra. Sasa Wayahudi, Waislamu, na Waprotestanti huabudu bila kizuizi. Na Mashahidi wa Yehova hawako tena chini ya marufuku. Madrid inajivunia msikiti mpya na sinagogi moja, pamoja na ofisi ya tawi ya Mashahidi wa Yehova katika Uhispania. Kukiwa na zaidi ya washiriki watendaji 90,000, Mashahidi huonwa kuwa dini kubwa zaidi isiyo ya Kikatoliki katika Uhispania.

Ikiwa ungependa habari zaidi kuhusu Mashahidi wa Yehova na imani zao, tafadhali andikia I.B.S.A., Box 47788, Nairobi, Kenya, au tumia anwani ifaayo iliyoorodheshwa kwenye ukurasa 5.

[Picha katika ukurasa wa 32]

Ofisi ya tawi ya Watch Tower Society ya Uhispania.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki