Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 2/8 kur. 28-29
  • Kuutazama Ulimwengu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kuutazama Ulimwengu
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Katekisimu Mpya ya Kikatoliki_
  • Je! Urefu wa Maisha Ulioongezeka ni Baraka?
  • Ili Kuokoa Kolosiamu
  • ‘Hakuna Mapadri—Hakuna Kanisa’
  • Infleshoni Huharibu Maadili
  • Steroidi kwa Ajili ya Sura
  • Mitazamo Kuelekea UKIMWI
  • Nguvu za Mwezi
  • Kisababishi cha Ugonjwa wa Safari Chagunduliwa
  • Wenye Umri wa Makamo Wapoteza Kazi
  • Jitihada za Kupendwa na Wengi Zaleta Matokezo Yaliyo Kinyume
  • Ninapaswa Kujua Nini Kuhusu Dawa za Steroidi?
    Amkeni!—2005
  • Je! Katekisimu Mpya Itabadili Mambo?
    Amkeni!—1993
  • Takwimu za UKIMWI Zenye Kushtua!
    Amkeni!—2001
  • UKIMWI Katika Afrika—Jumuiya ya Wakristo Ina Lawama Kadiri Gani?
    Amkeni!—1996
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 2/8 kur. 28-29

Kuutazama Ulimwengu

Katekisimu Mpya ya Kikatoliki_

Vatikani imetangaza kwamba baada ya miaka sita ya utayarishaji, itatoa karibuni katekisimu mpya ya kutumiwa ulimwenguni pote. Hii ndiyo mara ya pili tu katika historia ya Kanisa Katoliki kwamba katekisimu imetolewa. Katekisimu ya kwanza ya kutumiwa ulimwenguni pote ilitolewa katika 1566, kufuatia Baraza la Trent, na ilikuwa sehemu ya jitihada ya kanisa ya kupinga matokeo ya Mapinduzi Makubwa ya Kanisa. Gazeti la Ufaransa Le Monde lasema kwamba katekisimu hiyo ni ishara ya “kukubalia kundi lenye kushikilia mapokeo ambalo limekuwa likifanya kampeni tangu Vatikani 2 ili kupata katekisimu moja ya pekee yenye kuonyesha kanuni za kale zaidi, zilizo za kimapokeo zaidi.” Katika kutoa kibali chake rasmi kwa maandishi, Papa John Paul 2 alisema kwamba katekisimu hiyo mpya “ingeandaa kitu imara cha marejezo katika kutayarisha katekisimu za kitaifa na za kiparishi.”

Je! Urefu wa Maisha Ulioongezeka ni Baraka?

Ijapokuwa sayansi ya tiba imeongeza wastani wa tarajio la maisha ya mwanadamu kwa kadiri fulani katika miaka ya karibuni, Dakt. Hiroshi Nakajima, mkurugenzi mkuu wa WHO (Shirika la Afya Ulimwenguni), akubali kwamba “afya na ubora wa maisha ya idadi ya watu ulimwenguni havina maendeleo hata kidogo.” Katika mahoji na gazeti la Paris Le Figaro, Dakt. Nakajima alisema hivi: “Kulingana na habari yetu, idadi ya wagonjwa au walemavu, hasa miongoni mwa wenye umri mkubwa, huenda hata ikawa imeongezeka. “Duniani pote, wastani wa tarajio la maisha sasa ni miaka 65. Katika nchi zilizositawi kiviwanda ni miaka 76, hali katika nchi zinazositawi wastani ni miaka 62, na ni miaka 50 tu katika maeneo ya dunia ambayo yamesitawi kidogo sana. Katika miaka mitano ijayo, WHO latumaini kuongeza wastani wa tarajio la maisha kwa miezi minne. Lakini Dakt. Nakajima asema hivi: “Ni wazi kwamba maongezeko katika urefu [wa maisha] hayamaanishi maisha bila ulemavu au magonjwa yenye kusedeka.”

Ili Kuokoa Kolosiamu

“Roma yasimama, maadamu Kolosiamu yasimama,” yasema mithali moja ya kale ya Kilatini. Hata hivyo, kupenya kwa maji ya mvua, utendaji wenye kuharibu wa uchafuzi wa angahewa, na mitetemo yenye kusababishwa na magari ya jiji vimetia jengo hilo la ukumbusho lenye kujulikana sana katika hali ya hatari. Vipande huanguka kutoka kwalo kila siku, na mahali kadhaa pahitaji kuimarishwa. Ili kuokoa jengo hilo kubwa la michezo lisiharibike zaidi, maafikiano yamefikiwa kati ya Wizara ya Italia ya Urithi wa Kitamaduni na benki moja ya Roma. Sehemu ya kwanza ya mradi huo yatia ndani kulikinga na maji na kurejesha matao na kujenga upya sakafu ya mbao ya uwanja huo, ambamo watu walikuwa wakipigana hadi kufa wakati mmoja. Likirejezea utumizi huo uliopangwa wa lira bilioni 40 (dola milioni 32 za U.S.), gazeti La Repubblica huyaita maafikiano hayo “muungano mkubwa zaidi kati ya sehemu za umma na za faragha uliopata kufanywa ili kuokoa kazi ya sanaa.”

‘Hakuna Mapadri—Hakuna Kanisa’

Makasisi wa Kikatoliki katika Ufaransa wanakabili tatizo zito—uzee. Kukiwa na mapadiri wapya wachache mno ili kujaza nafasi zinazoachwa wazi na makasisi wenye umri mkubwa wanaopotezwa kupitia kifo au kustaafu, idadi ya mapadri katika Ufaransa inazidi kupungua. Gazeti Ouest-France laripoti kwamba katika Brittany, ngome ya kimapokeo ya Kikatoliki katika magharibi mwa Ufaransa, idadi ya mapadri imeshuka kufikia 2,207 tu. Ni mapadri 180 walio na umri ulio chini ya miaka 50, kati yao 900 wana umri wa kati ya miaka 50 na 70, na zaidi ya nusu wana umri wa zaidi ya miaka 70. Akitabiri kwamba mwelekeo huo ungemaanisha hatari kwa kanisa, askofu mkuu wa Rennes, Jacques Jullien, aliomboleza hivi: “Upungufu wa mapadri ndilo tatizo letu namba moja. . . . kuwa hakuna mapadri kwamaanisha kuwa hakuna kanisa.”

Infleshoni Huharibu Maadili

Kiasi kikubwa cha infleshoni kwa kipindi kirefu cha wakati kina matokeo gani juu ya watu? Katika kujibu swali hilo lililoulizwa na gazeti Veja, mtaalamu wa uchumi Eduardo Giannetti da Fonseca wa Chuo Kikuu cha São Paulo alijibu hivi: “Infleshoni huathiri viwango vya kiadili vya jamii. Nchi ambako watu hawajui pesa zilizomo mfukoni mwao zitakuwa na thamani gani mwezi ujao mwishowe huridhiana na kanuni za kiadili za msingi kabisa za mahusiano ya kibinadamu. Utumainifu, kweli, kuwahi, unyoofu, na uaminifu-mshikamanifu hudhoofishwa na ukosefu wa uthabiti wa kiuchumi.” Katika kujihami dhidi ya gharama ya juu ya maisha, serikali na watu wa kawaida huenda wakahisi kwamba matokeo hustahilisha njia zilizotumiwa. Asema Fonseca: “Infleshoni ni shule ya utumiaji fursa kujifaidi binafsi, kutaka vitu papo hapo, na ufisadi.”

Steroidi kwa Ajili ya Sura

Utumizi wa steroidi anaboliki (madawa ya kujenga misuli) na wanariadha watumainio kuongeza utendaji wao wa kiriadha umejulikana kwa muda mrefu. Hata hivyo, katika miaka ya karibuni matumizi mabaya ya steroidi yamesambaa miongoni mwa wasio wanariadha kwa makusudi ya uzuri wa sura. Uchunguzi mmoja ulioripotiwa na Shirika la Afya Ulimwenguni uliona kwamba miongoni mwa wanafunzi wa madarasa ya juu katika shule za sekondari katika United States, asilimia 6.6 ya wanaume wote walikuwa wametumia steroidi. Kati ya kikundi hicho asilimia 26 walisema kwamba sababu yao kuu ya kutumia steroidi ilikuwa kufanyia maendeleo sura yao. Athari mbaya za kutumia steroidi anaboliki hutia ndani kolesteroli iliyoongezeka, kujazana maji katika tishu, na hatari kubwa zaidi ya ugonjwa wa mshipa koronari, kuongezeka ukubwa kwa tezi-shahawa, vivimbe vya ini, kufinyaa kwa tezi-shahawa, na kutoweza kwa wanaume kufanya ngono. Steroidi zafikiriwa pia kuwa zachochea mwendo wenye uchokozi, wenye kutaka vita.

Mitazamo Kuelekea UKIMWI

“Waafrika Kusini wengi hushindwa kuona umaana wa [UKIMWI] au hukataa kuamini kwamba ugonjwa huo uko kabisa,” laripoti Saturday Star la Johannesburg, Afrika Kusini. “Mchanganyiko hatari wa ubaguzi wa rangi, umaskini na ujinga vinaongeza mweneo wa maradhi hayo yasiyoponyeka.” Baadhi ya watu huhisi kwamba wazo la UKIMWI ni hila ya Magharibi ya kudhoofisha Afrika au kwamba maradhi hayo ni ubuni fulani wa watu weupe ili kuzuia mwendo wa uzazi wa watu weusi wa Afrika. Jambo jingine linaloathiri mtazamo wa watu kuelekea UKIMWI ni jeuri ambayo imekuwa sehemu ya maisha ya kila siku kwa wengi. Mwanamume mmoja wa Afrika Kusini katika eneo moja lenye kusumbuliwa na vita alikiambia hivi kikundi kimoja cha washauri juu ya UKIMWI: “Mwaniambia kwamba UKIMWI waweza kunifanya mgonjwa katika muda wa miaka 10. Lakini watu 25 walikufa hapa . . . mwisho-juma uliopita [katika jeuri ya kisiasa]. Je! kweli UKIMWI ungeweza kufanya maisha kuwa mabaya zaidi ya yalivyo tayari?” Maoni yasipobadilika, inakadiriwa kwamba maradhi hayo yataongezeka sana katika Afrika Kusini katika muda wa miaka 10 hadi 15 ifuatayo.

Nguvu za Mwezi

Imejulikana kwa muda mrefu kwamba mwezi husababisha kupwa na kujaa kwa maji ya bahari za dunia. Hata hivyo, gazeti ya Kifaransa Terre Sauvage huripoti kwamba wanasayansi kutoka CNRS (Kituo cha Utafiti wa Kisayansi cha Taifa cha Ufaransa) sasa chathibitisha kwamba mwezi una matokeo kama hayo juu ya uso wa ardhi ya dunia. Kwa njia ya chombo cha uchunguzi kilichowekwa katika dimbwi la maji ya chumvi katika pango lililozibwa ambalo liko meta 1,000 chini ya ardhi, watafiti waliweza kugundua hali ya kuinuka na kuanguka kwa vitu vilivyokuwamo ndani ya pango hilo kila saa 12. Mwendo huo, uliosababishwa na kupanuka na kusongamana kwa kuta za pango hilo, hulingana na mwendo wa mwezi kuzunguka dunia nao huthibitisha kwamba kwelikweli mwezi ndio chanzo cha kile ambacho Terre Sauvage huita “kupumua kwenye kushangaza chini ya ardhi.”

Kisababishi cha Ugonjwa wa Safari Chagunduliwa

Watu wengi zaidi wamepatwa na ugonjwa wa mwendo wakati fulani maishani mwao. Mamilioni hupatwa nao kwa ukawaida wasafiripo. Sasa wanasayansi waamini kwamba wanaelewa kinachochochea hali ya kuchafuka moyo. Tatizo linakuwa katika ubongo, ambapo habari inayopelekwa na macho hailingani na habari inayohisiwa na sikio la ndani. Mathalani, sikio la ndani huhisi mwendo wa mwili ndani ya mashua inayosukwasukwa hali macho huona mandhari yenye kutulia huku mwili ukienda pamoja na mashua. Ujumbe huo unaopingana wenye kupokewa na ubongo husababisha kuachiliwa kwa homoni zinazohusiana na mkazo na ongezeko la mwendo wa mipigo ya kielektriki katika misuli ya tumbo, na baada ya wakati, hiyo hutokeza kuchafuka moyo na kutapika. Njia za kuepuka ugonjwa wa mwendo hutia ndani kula mlo kidogo wenye wanga, usio na mafuta mengi, kabla ya kusafiri; kutazama vizingo vya barabara yenye kupinda unapokuwa katika gari au kwenye upeo wa macho unapokuwa katika mashua ili macho yako yaweze kuona kile kinachohisiwa na sikio lako la ndani; kupunguza mwendo wa kichwa na mwili; na kushughulisha akili kwa mawazo mengine.

Wenye Umri wa Makamo Wapoteza Kazi

“Ikiwa wewe una zaidi ya [miaka] 40, usifikirie hata kubadili kazi yako,” lasema The Star, gazeti la Johannesburg, Afrika Kusini. Wafanyakazi wengi katika Afrika Kusini wanaachishwa kazi likiwa tokeo la kupungua kwa uchumi. Wa kwanza kupoteza kazi zao mara nyingi ni watu wa umri mkubwa ambao wanakaribia umri wa kustaafu. Kulingana na tarakimu kutoka Idara ya Leba, watu 37,500 wenye umri wa zaidi ya [miaka] 50 wanapoteza kazi zao kila mwezi katika Afrika Kusini. “Hali hiyo ya Afrika Kusini si tofauti na mielekeo ya ng’ambo ambako si wanaume na wanawake wengi wenye umri wa [miaka] 55 na zaidi wangali wanafanya kazi,” lasema The Star. “Shirika kwa Ajili ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo lasema kwamba kuajiriwa kazi kikawaida kwa wanaume na wanawake wenye umri wa [miaka] 55 na zaidi sio mwelekeo wenye kufuatwa sana. . . . Tofauti ni wanaume wenye umri mkubwa wa Japani, asilimia 60 yao hufanya kazi.”

Jitihada za Kupendwa na Wengi Zaleta Matokezo Yaliyo Kinyume

Jitihada za karibuni za wanasiasa wa U.S. kujipatia upendeleo kwa kuongeza mambo ya kidini katika kampeni zao zimekuwa na matokeo yaliyo kinyume. Katika kisa kimoja, msikilizaji aliandikia Daily News la New York hivi: “Jesse Jackson ahitaji kutumia Biblia yake. Katika hotuba yake kwenye mkusanyiko wa Demokrasia Julai 15, alisema juu ya Maria na Yusufu kuwa wenzi wasio na makao na Maria kuwa mama mseja. Maria na Yusufu hawakuwa ‘wenzi wasio na makao.’ Walisafiri kwenda Bethlehemu ili kutimiza sheria, walikimbilia Misri ili kuepuka mnyanyaso wa Herode, lakini waliishi Nazareti. Na Maria hakuwa ‘mama mseja.’ Katika Mathayo Sura 1, mistari 18-23, na katika Luka, Sura 1, mistari 26-35, Yusufu hurejezewa kuwa mume wa Maria na Maria kuwa mke wa Yusufu. Hivyo, ingawa ‘wasio na makao’ na ‘mseja’ ni vivumishi vyenye kupendwa na wengi vyenye matokeo, havitumiki, katika kisa hiki. Jesse, hakikisha una mambo hakika na ya kweli.”

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki