Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 3/22 uku. 31
  • Mchekeshaji Mwenye Manyoya wa Ziwa Viktoria

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Mchekeshaji Mwenye Manyoya wa Ziwa Viktoria
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • “Mkazi wa Msituni Mwenye Kuvutia Kuliko Wote”
    Amkeni!—2000
  • Ziwa Viktoria—Ziwa Kuu la Afrika
    Amkeni!—1998
  • Kumlea Mtoto Porini
    Amkeni!—2001
  • Mbayuwayu Mwenye Kuruka kwa Kasi
    Amkeni!—1999
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 3/22 uku. 31

Mchekeshaji Mwenye Manyoya wa Ziwa Viktoria

Na mleta habari za Amkeni! kutoka Kenya

MASHUA yetu inaenda kasi katika maji maanana ya Ziwa Viktoria wakati ghafula kinapoonekana. Kati ya panda kuu ya mti mzee unaoenea hadi juu ya ziwa, mna kiota kikubwa cha ndege. Kina kipenyo cha mita 1.8—kikubwa vya kutosha kuzusha hofu kwamba kiumbe cha kipterodaktali (cha hekaya ya kale) lazima kiwe kinaishi kwenye kiota hicho.

Hata hivyo, tukiazimia kuona kiota hicho, tunafunga mashua yetu kwenye mwamba mkubwa karibu na msingi wa mti huo mkubwa, na sisi sote tunapanda hadi kwenye panda ili kukiona vizuri. Wote, yaani, isipokuwa nahodha wetu. Watu wanaoishi kando ya ziwa hilo huepuka ndege huyo kwa vyovyote. Hata jina lake linatisha—nyundo (mshingi)!

Tunapokaribia kiota, tunaona kuwa hakifanani na kiota kingine chochote ambacho tumeona. Huchukua nyundo wa kiume na kike siku tatu hadi nne za kazi ngumu kujenga tu “msingi” wa kao lao—jukwaa lililojengwa kiholela kidogo, lenye umbo la kijisahani. Limejengwa kwa nyasi, vijiti, na majani makavu. Ujenzi huo ukisha kamilika, wao hujenga kuta kulizunguka na kisha kuanza kujenga paa kutoka nyuma. Paa linapofikia nusu likamilike, nyundo wa kike hustarehe nyumbani. Atakaa katika kiota huku yule wa kiume akitafuta vifaa zaidi vya kujengea.

Baada ya sehemu ya mbele kumalizika, wao hutia tabaka ya udongo juu yayo na katika chumba cha ndani. Kisha vitu mbalimbali huongezwa kwenye pande na paani ili kufanya kiota kisivuje maji na kiwe na joto. Hatimaye, nyumba yao “hurembeshwa.” Mikebe, ngozi za nyoka, vitambaa—kwa kweli chochote ambacho nyundo wa kiume aweza kupata—huongezwa juu ya kiota. Kazi yote huchukua muda wa majuma matano au sita.

Tulipomaliza kuchunguza kiota, tulipanda tena mashuani na kungoja. Haikuwa muda mrefu kabla ndege nyundo kutokea kwa utukufu, akitua juu ya paa. Lakini kwa mshangao wetu, huyo si ndege jitu. Ana urefu wa sentimita 56 tu, mwenye rangi kahawia, na sura ya kawaida. Yaani, isipokuwa kichwa chake. Mdomo mkubwa na kishungi kikubwa kisogoni humpa sura ya kichwa cha nyundo. Ndiposa huitwa nyundo.

Halafu kidogo nyundo aanza utaratibu ambao umempatia sifa yake kuwa mchekeshaji mwenye manyoya. Yeye atoa mteteo wa sauti ya juu na aanza kucheza dansi na kuruka-ruka huku na huku. Ghafula mwenzi wake atokea na kuungana naye kwa kuruka mgongoni mwake na kujiunga katika usanii huo wa kucheza dansi wenye kuchekesha. Hata hivyo, utaratibu huo wa ndege huyo haujamalizika. Sasa anaruka chini ghafula kutoka kwa kao lake la kando ya ziwa na kutua mgongoni mwa kiboko anayelala. Kiboko huyo anaposonga, sakafu ya ziwa yenye matope huvurugwa. Vyura walioshtuliwa huogelea hadi juu ya maji—na kukamatwa na nyundo. Samaki wadogo, nyungunyungu, wadudu, na wanyama wenye magamba ni baadhi ya chakula cha nyundo.

Iwe utamwita mchekeshaji au mjenzi stadi, nyundo huvutia—mfano mwingine wa ubuni usio na mpaka wa Muumba wetu.

[Picha katika ukurasa wa 31]

Nyundo na kiota chake

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki