Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 3/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 3/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

KULEA WATOTO Ule mfululizo “Watoto wako—Kufanya Yale Yanayowafaa Zaidi” (Septemba 22, 1992 Kiingereza) ulifunua upungufu wangu nikiwa mzazi. Fikira zangu zimekuwa zikielekezwa kwa mambo ya kibinafsi na utendaji wa kundi—na kumpuuza mwana wangu mwenye miaka mitatu. Alikuja kuwa mtoto asiyetulia hata kidogo. Pia mimi huelekea kuwa mwenye hasira, mwenye kukasirika upesi, na mwenye haya kuonyesha shauku. Badala ya kumkumbatia mwanangu, nimepita kiasi katika kujaribu kuwa mkali. Kwa kuwa Yehova hutuonyesha sisi sote upendo bila kujizuia, sasa nitajaribu kuonyesha upendo urithi niliopokea kutoka kwa Yehova.

T. T., Japan

Ingawa mimi si mzazi, mimi hupenda watoto, na toleo hilo liligusa moyo wangu. Nililia kujua juu ya matatizo ya kuhuzunisha ambayo watoto hukabili leo. Makala yenu ilitoa habari nyingi pia katika kuonyesha jinsi ya kushughulika na matatizo hayo katika sehemu za kwanza kabisa za maisha ili kuepuka matatizo makubwa katika miaka ya baadaye.

L. B., United States

Makala hiyo ilinifanya nijitahini nikiwa baba. Nilipooa, nilikuwa mchanga mno na nilipendezwa zaidi kuwa na marafiki wangu kuliko kuwa na familia yangu. Kusoma makala hizo kulinifanya ning’amue kwamba sikutumia wakati wa kutosha pamoja na binti yangu. Makala hiyo na isukume wazazi wafanye yale yanayowafaa watoto wao zaidi.

A. V., Italia

Hadithi za Wanyama Asanteni kwa makala “Mgugunaji wa Amerika (Capybara)—Kosa au Muujiza wa Uumbaji?” (Septemba 22, 1992 Kiingereza) Mara nyingi mimi humsomea mtoto wangu makala za wanyama. Huku Bwa. Capybara mwenyewe akiwa anazungumza, makala hiyo ilimpendeza mwanangu!

C. T., Japan

Lilikuwa jambo tofauti lenye kuburudisha kwa kulinganisha na habari duni ya magazeti mengi! Watoto wangu nami tuliisoma pamoja. Kujifunza juu ya wanyama wapya walio tofauti kulifurahisha!

C. H., United States

Asanteni kwa makala “Wanyama Pochi Wenye Kustaajabisha wa Kutoka Chini.” (Julai 22, 1992 Kiingereza) Nilipendezwa hasa na jinsi ambavyo wanyama hao huzaa na kutokeza maziwa aina tofauti. Kulinifanya nifikiri jinsi uwezo wa Yehova unavyoonekana wazi katika uumbaji wake!

N. S., Italia

Nina miaka 14, na nilifurahia makala “Ngamia wa Uarabuni—Gari la Afrika Lenye Matumizi Mengi.” (Juni 8, 1992 Kiingereza) Mlisimulia mambo kwa njia iliyofanya habari hiyo iwe yenye kusisimua sana.

G. C., Argentina

Kusema Mbele ya Watu Makala “Wewe Waweza Kusema Mbele ya Wasikilizaji!” (Julai 22, 1992 Kiingereza) ilinisaidia kupata kazi. Niliisoma kwanza nikiwa na kusudi la kuitumia katika huduma ya Kikristo. Lakini nilipojulishwa juu ya kuhojiwa juu ya kazi, niliisoma makala hiyo tena na kutumia mambo mengi yaliyotajwa, kama vile mazoezi ya kupata utulivu. Kisha nikatoa sala na nikaenda kwenye mahoji hayo. Niliipata kazi hiyo, na ninawashukuru kwa kuandaa makala hiyo kwa wakati unaofaa.

K. B., United States

Uvumbuzi wa Anga Nikiwa msomaji mwenye bidii wa mabuniko ya sayansi, nilisisimuliwa sana na mfululizo wa uvumbuzi wa anga (Septemba 8, 1992 Kiingereza) Ilinipatia maoni yaliyosawazika juu ya mada hii yenye kupendeza. Pia ilitia moyo kuona kwamba Mungu ana kusudi zuri ajabu si kwa ajili ya sayari hii tu bali kwa ulimwengu wote mzima.

A. C., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki