Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 3/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 3/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kuwapa Watoto Nidhamu Nilithamini kwelikweli makala “Maoni ya Biblia . . . ‘Fimbo ya Nidhamu’—Je! Ni ya Kishamba?” (Septemba 8, 1992 Kiingereza) Watoto wakitendwa vibaya na kukiwa na ukatili mwingi ulimwenguni, tunahitaji makala kama hiyo ili itusaidie tubaki wenye usawaziko. Ninawajua watoto waliotendwa kwa ukali wenye kupita kiasi tangu utoto. Leo wao ni vijana matineja wenye matatizo makubwa ya kihisiamoyo. Tunahitaji habari kama hiyo ili kutusaidia kuongoza na kufundisha watoto wetu kwa njia yenye upendo.

. B., United States

Nguo za Washonaji Stadi Asanteni kwa makala “Vijana Wanauliza . . . Nguo za Washonaji Stadi—Zinanifaa?” (Septemba 8, 1992 Kiingereza) Nilipoacha kazi yangu mwaka uliopita ili kuwa mweneza evanjeli wa wakati wote, singeweza tena kununua nguo za washonaji stadi. Hilo lilinihuzunisha kwa muda fulani. Hata hivyo, sasa ninaweza kuona kwamba chaguo nililofanya lilifaa na kwamba nguo za kuonyesha ufanisi wa mtu hazikunifaa.

. J. C., Brazili

Msiba wa Bahari ya Aral Asanteni sana kwa makala “Msiba wa Bahari ya Aral.” (Agosti 22, 1992 Kiingereza) Tangu nilipokuwa shuleni, bahari hii ya barani, pamoja na Bahari Caspian iliyo karibu, zimenivutia. Kwa muda wa miaka, nimeweza kukusanya habari kuhusu ni ipi iliyo kubwa kati ya hizo mbili, lakini isipokuwa makala yenu, habari kuhusu Bahari Aral zilikuwa chache na nadra sana.

D. H., Ujerumani

Nyanya na Babu Ingawa sisi si vijana tena, mke wangu nami tumethamini sana makala za “Vijana Wanauliza . . . ” juu ya kuishi na nyanya na babu. (Julai 8 na Julai 22, 1992 Kiingereza) Hivi karibuni tulihamia kwa nyanya ya mke wangu, na hiyo imetuletea magumu kwelikweli. Shauri lenu la Biblia na mwono-ndani wa hekima kwa watu wazee ulikuwa jambo tulilohitaji. Mafunzo mawili ya familia yakitegemea makala hizo na utumizi halisi wa shauri ulifanya hali yetu iwe na maendeleo.

J. L., United States

Midundo Mizito Makala yenu “Midundo Mizito—Ujumbe ni nini?” (Julai 8, 1992 Kiingereza) ilinivutia sana. Nimekuwa nikivurugika akili kwa sababu ya muziki huo. Makala yenu ilinipa nguvu na ujasiri wa kutupilia mbali muziki huo wa kishetani. Bado ni mng’ang’ano mkubwa, lakini kwa msaada wa Yehova nitaweza kushinda.

M. D., United States

UKIMWI Makala yenu “UKIMWI Barani Afrika” (Agosti 8, 1992 Kiingereza) ilikuwa yenye kutegemeka sana! Shauri kwa vijana wanaofikiria ndoa laweza hata kuwa lenye kuokoa uhai. Mimi ni Mkristo aliyebatizwa karibuni, na kwa sababu ya mtindo-maisha wangu wa kale, nilienda kupimwa kuona ikiwa nina ambukizo la HIV. Sikuwa nalo. Ninashangaa kwa nini wengine wanaopaswa kupimwa hawafanyi hivyo. Wengi waliofunga ndoa ambao wenzi wao wamekuwa wasio waaminifu wanatumaini tu kupata mazuri. Lakini hali inakuwa ya hatari zaidi kuweza kukaa tu na kutumaini kwamba hawajaambukiwa ugonjwa huo hatari.

L. J., United States

Tunathamini maelezo hayo ya waziwazi. Kulingana na Vituo vya U.S. vya Udhibiti wa Magonjwa, inaweza kuchukua kutoka miezi mitatu hadi sita baada ya kuambukiwa ili mwili utokeze mazindiko ya kutosha kuweza kugunduliwa kwa kupimwa HIV. Hivyo kupimwa tena ni jambo la busara ikiwa kupimwa huko kunafanywa muda mfupi baada ya kuambukiwa virasi ya UKIMWI.—Mhariri.

Nilitaka tu kutoa shukrani kwa makala “UKIMWI—Wafanyakazi Watahadhari!” (Juni 22, 1992 Kiingereza) Mimi hufanya kazi katika kituo cha matibabu ya dharura. Muda mfupi baada ya kusoma makala hiyo, nilifanya mkutano wa wafanyakazi ambapo tahadhari hizohizo zilizungumzwa kirefu. Niliweza kuwaambia wengine kwamba nilikuwa nimesoma hayo kwanza katika Amkeni!

T. M., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki