Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 5/22 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 5/22 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Masuala ya Wanawake Asanteni sana kwa makala zinazozungumzia kupigwa kwa wanawake (Novemba 22, 1988, Kiingereza), msaada kwa familia za walevi (Mei 22, 1992, Kiingereza), na staha kwa wanawake (Desemba 8, 1992). Makala hizo zaonyesha uelewevu wa ajabu wa akili ya binadamu. Katika usiku wa arusi yangu, niliingizwa katika matatizo mengi sana ya kufadhaisha. Nilianza kuwa na matatizo ya afya na nikawaona madaktari na washauri wa matatizo ya akili. Wengi hawawezi kuelewa jambo kama hilo kwa urahisi, na ukimwendea yeyote akusaidie na asijue jambo la kusema, inakuwa vigumu hata zaidi. Kwa vyovyote vile, hatimaye ninahisi kwamba matatizo hayo yametatuliwa kabisa, asanteni kwa makala zenu.

N. H., Argentina

Niagara Nilishindwa kujizuia kutabasamu nilipokuwa nikisoma ile makala ya “Maporomoko ya Niagara—Johari ya Kale ya Amerika.” (Oktoba 8, 1992, Kiingereza) Tuna maporomoko madogo-madogo ya maji huku katika msitu, lakini wazo la uzuri kama huo wa ajabu lilinifanya nifikirie upendo wa Yehova kwetu na tamaa yake ya kutufanya tuwe na uthamini sana kwa uumbaji wake.

P. J. O., Naijeria

Kustahi Wanawake Wakati wa utoto wangu, niliiga ubaguzi wa kijamii hivi kwamba nikawa mwenye kuchukia wanawake sana. Nisingefikiria ndoa! Lakini kwa sababu ya mfululizo wa makala zenye kichwa “Wanawake—Wanastahili Staha” (Desemba 8, 1992), nimebadili maoni yangu kuelekea wanawake. Nilisoma makala hizo mara mbili, na sasa ninafikiri kwamba siku moja naweza kuwa mume mwema.

N. B. M., Côte ď Ivoire

Mazungumzo ya Simu Nilivutiwa na makala yenu ya “Vijana Wanauliza . . . Kuna Ubaya Gani Kuongea Pamoja?” (Agosti 22, 1992, Kiingereza) Mimi pia nilikuwa nikizungumza na mmoja wa jinsia tofauti katika simu. Nilijawa sana na mapenzi! Lakini nilipokabili mtu huyo na kumweleza hisi zangu, niligundua kwamba hakunifikiria kwa uzito. Nilikuwa nimebembwa. Laiti ningalikuwa nimesoma makala yenu mwaka mmoja uliopita. Huenda moyo wangu usingeumizwa sana hivi.

L. R., United States

Uvumbuzi wa Angani Nafanyia kazi tawi la Italia la Shirika la Anga la Ulaya. Nimedokeza zaidi ya mara moja kwamba broshua ya matangazo inayotayarishiwa wafanyakazi wetu itie ndani makala za kutoka Amkeni!—lakini bila kufanikiwa. Hata hivyo, zile makala “Uvumbuzi wa Angani” (Septemba 8, 1992, Kiingereza) zilitumiwa na zikachukua karibu nafasi yote ya broshua hiyo ya matangazo! Asante kwa Amkeni! Nimekuwa na fursa nyingi za kuzungumzia Biblia na wenzangu kazini.

P. B., Italia

Vitumbuizo Nina miaka 20 na nimetoka tu kumaliza zile makala “Vitumbuizo Vinaathirije Maisha Yako?” (Novemba 8, 1992, Kiingereza) Niliona habari hiyo kuwa ya wakati unaofaa na yenye kusawazika. Vijana wengine huona kama wamebanwa na vizuizi vyote na miongozo ambayo ni lazima tufuate tukiwa Wakristo. Kwa mfano, ndugu yangu aliacha kuwa Mkristo kwa sababu alihisi hivyo. Lakini naiona miongozo hiyo kuwa ulinzi, nami nahisi kuwa salama na kupendwa nikijua kwamba Yehova anatujali sana hivi kwamba anatutenganisha na ulimwengu wa Shetani.

D. C., United States

Nilithamini sana lile toleo la vitumbuizo, lakini ningependa kujua mnapata wapi habari inayowawezesha kueleza kindani sinema kama Basic Instinct?

A. A., Italia

Maelezo hayo yalitegemea ripoti za habari katika magazeti mashuhuri. Haikuwa lazima washiriki wa wafanyakazi wetu wa utafiti watazame sinema isiyofaa kama hiyo.—MHARIRI.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki