Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 1/8 uku. 30
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
  • Amkeni!—1993
  • Habari Zinazolingana
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
  • “Gazeti Hili la Amkeni! Liliandikwa kwa Ajili Yetu Haswa”!
    Amkeni!—1999
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1997
  • Kutoka kwa Wasomaji Wetu
    Amkeni!—1993
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 1/8 uku. 30

Kutoka kwa Wasomaji Wetu

Kesi za Mahakamani Nikiwa wakili anayehusika na kesi za haki ya kumtunza mtoto na za mashtaka ya damu, siwezi kueleza jinsi nilivyotiwa moyo sana na makala “Mashahidi wa Yehova ‘Wapelekwa Mbele ya Mahakama za Kwao.’” (Septemba 22, 1992, Kiingereza) Juma lililopita baadhi ya madaktari, wakipuuza maagizo hususa na kwenda kinyume, walimtia damu Shahidi. Huko kutojali haki za kidini na za kibinafsi kunachukiza. Makala yenu ilinitia moyo hata zaidi kuendelea kupigana vita!

P. P., United States

Wanawake—Wanastahili Staha Asanteni kwa mfululizo wa makala “Wanawake—Wanastahili Staha.” (Desemba 8, 1992) Ulinisaidia nielewe kwamba kuchukua wanawake kivivi-hivi si tatizo lililo katika jumuiya moja tu, lakini limo katika nchi nyingi. Pia ninashukuru kwa madokezo kuhusu kuepuka kuudhiwa kingono.

S. A., Naijeria

Ninathamini jinsi makala hizo zilivyo wazi. Madokezo yenu yatafanya watu wengi, wanaume kwa wanawake, wafikiri tena kuhusu mitazamo yao. Asanteni kwa kuonyesha jinsi Yehova huwaona wanawake.

J. P. L., Kanada

Kwa kweli ninahisi kwamba wanawake waliwekwa mahali pao panapofaa na walionwa kama vile wanavyopaswa kuonwa. Wanaume Wakristo na wathamini makala hizo pia ili kwamba, ikiwa inahitajika, waweze kubadili maoni yao kuhusu wanawake. Tutawaheshimu kwa unyoofu zaidi wakifanya hivyo.

E. S., Ufaransa

Makala hizo zinaturuhusu tujihisi vema zaidi na zaonyesha kwamba wanaume wana daraka la kutenda kwa amani na kwa staha kutuelekea. Ninafikiri makala hizo zilikuwa za ujasiri sana, na zinathaminiwa sana.

A. H., United States

Koo lilinikaba na nikalengwa na machozi machoni pangu kujua kwamba nimo katika tengenezo linalochukua msimamo imara kuhusu jinsi wanawake wanavyotendwa. Hizo ndizo makala za kwanza nilizopata kuona ambazo hazikuacha nafasi kwa wanaume wenye kututenda vibaya watumie kuwa kisababu.

E. M., United States

Ninajua kwamba habari hiyo kuhusu jinsi wanaume wanavyowaona wanawake haitabadili ulimwengu, lakini inatia moyo sana kusoma maneno ya kweli, ya faraja, ya huruma, na ya uelewevu, tukijua kwamba Yehova kwa kweli hutujali sisi.

H. Q., United States

Makala hizo ziliniathiri sana—si kwamba nimempuuza mke wangu, lakini nina uhakika ningeweza kufanya mengi kumsaidia. Ninamstahi sana na ninahisi kwamba makala hizo zitasaidia waume wote Wakristo watambue hata zaidi thamani ya wake zao. Wanastahili staha, fahari, upendo, na uelewevu kutoka kwa waume zao.

S. S., Brazili

Kifo Makala yenu kuhusu “Wakati Mpendwa Wako Anapokufa” (Julai 22, 1992, Kiingereza) ilinigusa moyo. Siku ileile tuliyoipokea, ndugu mkwe wangu mwenye miaka 16 alikufa kwa kansa. Makala hizo zilikuwa kitia moyo kwelikweli wakati wa taabu. Marafiki na familia yetu walikuja kutusaidia kwa kutuandalia chakula, faraja, na msaada katika kufanya mipango ya mazishi. Kwa kweli Yehova huandaa kitulizo kupitia makala za wakati unaofaa kama hiyo.

C. C., United States

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki