Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g93 7/8 kur. 26-27
  • Je! Unaweza Kutegemea Dhamiri Yako Iwe Kiongozi Chako?

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Je! Unaweza Kutegemea Dhamiri Yako Iwe Kiongozi Chako?
  • Amkeni!—1993
  • Vichwa vidogo
  • Habari Zinazolingana
  • Maana ya Dhamiri
  • Mbona Isifanye Kazi Vizuri?
  • Tunaweza Kufanya Nini?
  • Kuendelea Kuwa na Dhamiri Njema
    “Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
  • Dhamiri Njema Mbele za Mungu
    Jinsi ya Kudumu Katika Upendo wa Mungu
  • Je, Dhamiri Yako Imezoezwa Vizuri?
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—2005
  • Sauti ya Dhamiri Iliyomo
    Mnara wa Mlinzi Unaotangaza Ufalme wa Yehova—1975
Pata Habari Zaidi
Amkeni!—1993
g93 7/8 kur. 26-27

Maoni ya Biblia

Je! Unaweza Kutegemea Dhamiri Yako Iwe Kiongozi Chako?

UNAPOTEMBEA kwenye barabara yenye shughuli nyingi, unampita mwanamke aliyejivalia vizuri ambaye pasipo kujua anaangusha bunda la noti. Unapoinama ili uliokote, unamwona akiingia ndani ya gari kwa haraka. Utafanya nini? Je! utamwita kwa nguvu au utaingiza haraka noti hizo ndani ya mfuko wako?

Jibu lategemea dhamiri yako. Ingekuambia ufanye nini? La maana zaidi, je, unaweza kutumaini yale inayokuambia? Je! unaweza kwa usalama kuacha dhamiri yako ikuongoze?

Maana ya Dhamiri

Dhamiri imefafanuliwa kuwa hisia ya asili ya kujua mema na mabaya, yaliyo haki na yasiyo haki, ya adili na yasiyo ya adili. Biblia inaeleza utendaji wa dhamiri katika Warumi 2:14, 15: “Kwa maana watu wa Mataifa wasio na sheria wafanyapo kwa tabia zao yaliyo ndani ya torati, hao wasio na sheria wamekuwa sheria kwa nafsi zao wenyewe. Hao waionyesha kazi ya torati iliyoandikwa mioyoni mwao, dhamiri yao ikiwashuhudia, na mawazo yao, yenyewe kwa yenyewe, yakiwashtaki au kuwatetea.” Hivyo, dhamiri yako imefanyizwa iweze kukusaidia katika kuchanganua hali, kufanya uchaguzi unaofaa, na kujipima kwa uchaguzi wako ambao umefanya. Lakini, je, unaweza kuitumaini?

Jambo hilo linategemea. Isitoshe kuna ushuhuda wa kutosha wa kuthibitisha kwamba dhamiri yenye makosa inaweza kuongoza mtu katika mwenendo mbaya. Uhakika wa kwamba dhamiri ya mtu inakubali tabia ya aina fulani haithibitishi kwamba Mungu anairuhusu tabia hiyo. Kwa mfano, kabla awe Mkristo, Sauli wa Tarso aliongoza mnyanyaso wa Wakristo. Hata alikubali na kushiriki kabisa katika kuuawa kwa Mkristo mfia imani Stefano. Katika hayo yote, dhamiri yake haikumshutumu.—Matendo 7:58, 59; Wagalatia 1:13, 14; 1 Timotheo 1:12-16.

Katika Ujerumani ya Nazi wakati wa Vita ya Ulimwengu 2, askari wengi wa polisi wa SS walisema kwamba walikuwa wakifuata tu maagizo walipowatesa na kuua mamilioni katika kambi za mateso za Hitler. Dhamiri zao ziliwaruhusu wafanye hivyo. Lakini uamuzi wa ulimwengu—na la maa-na zaidi uamuzi wa Mungu—haukukubali matendo yao. Kwa haki, walihukumiwa.

Mbona Isifanye Kazi Vizuri?

Mbona kitu kilichoumbwa na Mungu kisifanye kazi vizuri? Biblia inaelezea. Kwa sababu ya mwanadamu kutumbukia dhambi kupitia kutotii kwa Adamu, dhambi inasemwa kuwa ‘inatawala,’ ikilazimisha watu kutii tamaa zayo. (Warumi 5:12; 6:12) Dhamiri ya mtu, ambayo mwanzoni ilikuwa kamilifu, ikapotoka; nguvu inayosukuma dhambi sasa inashindana nayo. (Warumi 7:18-20) Jambo hilo likaanzisha lile pigano ambalo sisi sote twalijua: “Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. . . . katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.”—Warumi 7:21-23.

Kwa kuongezea udhaifu huo tuliorithi, dhamiri zetu huathiriwa na nguvu za nje. Kwa mfano, mkazo wa marika kwa wazi ilipotoa au kukandamiza dhamiri za askari wa Nazi wa SS waliotajwa mapema. (Linganisha Mithali 29:25.) Na zaidi, kulisha akili kwa mambo yasiyofaa, kama vile mambo yasiyo adilifu na jeuri kwenye TV na katika sinema na vitabu, vilevile kunaathiri. Tukijihatarisha kwa mambo kama hayo kwa ukawaida, hatimaye hayataonekana kuwa mabaya, na dhamiri yetu itadhoofishwa. Kwa maneno mengine, “mazungumzo [mashirika, NW] mabaya huharibu tabia njema.”—1 Wakorintho 15:33.

Mtu akizoezwa kutambua na kustahi sheria za Mungu, dhamiri yake kwa wazi itakuwa kiongozi chenye kutegemeka zaidi kuliko kama hajazoezwa. Hata hivyo, hata mtu mwenye uelewevu na uthamini sana kwa njia za Mungu mara kwa mara huenda akapata dhamiri yake kuwa kiongozi kisichotegemeka kwa sababu ya dhambi iliyorithiwa na kutokamilika, na pia labda ushawishi kutoka nje.

Tunaweza Kufanya Nini?

Je! dhamiri inaweza kubadilishwa, ifanywe ili itambue upesi kanuni zinazofaa? Naam. Paulo aliwashauri Wakristo kwamba wangeweza kufanya hivyo ‘kwa akili zao, kwa kutumiwa, kuzoezwa kupambanua mema na mabaya.’ (Waebrania 5:11-14) Matumizi kama hayo na mazoezi yanatia ndani kujifunza Biblia, kufuatia kwa uangalifu kiolezo kilichoachwa na Yesu Kristo. (1 Petro 2:21, 22) Baadaye, tunapotumia akili zetu katika kufanya maamuzi, dhamiri zetu zitatuongoza zaidi na zaidi kutoka kwa mawazo na matendo mabaya na itatuchochea kufanya jambo lifaalo na lililo zuri.

Hata hivyo, hatupaswi kamwe kujiona kuwa waadilifu zaidi au kusema kwamba kama jambo “halisumbui dhamiri yangu,” basi ni sawa. Matumizi yanayofaa ya dhamiri yanaweza kufananishwa vizuri na vitendo vya kutahadhari vya dereva anayeendesha salama. Dereva anapotaka kubadilisha leni barabarani, bila kufikiria ataangalia kioo kinachoona nyuma. Akiona gari, anajua kwamba ni hatari kwenda kwenye leni nyingine barabarani. Hata hivyo, hata kama haoni chochote, dereva mwenye akili anatambua kwamba kuna sehemu ambayo haoni—si kila kitu kinaweza kuonekana nyakati zote kwa kutegemea kioo. Kwa hiyo, hatazami tu kioo. Ageuza kichwa kuchunguza, akihakikisha kwamba leni hiyo ya barabara haina kitu kabla ya kuingia. Jambo hilo linafanana na dhamiri yetu. Ikikuonya, sikiliza! Lakini hata isipokuonya kwanza, uwe kama yule dereva mwenye hekima—chunguza kwanza uhakikishe kwamba hakuna hatari.

Chunguza fikira zako uone kama zinapatana na fikira za Mungu. Tumia Neno lake kuwa msingi wa kuchanganua dhamiri yako. Mithali 3:5, 6 husema hivi kwa hekima: “Mtumaini BWANA [Yehova, NW] kwa moyo wako wote, wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.”

Kwa hiyo ni jambo la hekima kusikiliza dhamiri yako. Lakini ni jambo la hekima hata zaidi kulinganisha mambo yote tunayofanya na mapenzi ya Mungu kama yalivyofunuliwa katika Neno lake. Ni wakati huo tu ndipo tunapoweza kusema kwa uhakika, “tunaamini kwamba tuna dhamiri njema.”—Waebrania 13:18; 2 Wakorintho 1:12.

[Picha katika ukurasa wa 26]

“Kuongolewa kwa Mtakatifu Paulo”

[Hisani]

Imechorwa na Caravaggio: Scala/Art Resource, N.Y.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki